Revised Common Lectionary (Complementary)
Maonyo Kwa Wanaomkataa Yesu
(Mt 11:20-24)
13 Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida![a] Watu wenu wameniona nikifanya miujiza mingi ndani yenu, lakini hamkubadilika. Miujiza hiyo hiyo ingefanyika katika miji ya Tiro na Sidoni,[b] watu katika miji hiyo wangelikwisha badili mioyo na maisha yao siku nyingi. Wangelikwisha vaa nguo za magunia na kukaa kwenye majivu kuonesha kusikitika na kutubu dhambi zao. 14 Lakini itakuwa rahisi kwa miji ya Tiro na Sidoni siku ya hukumu kuliko ninyi. 15 Nawe Kapernaumu, Je! Utatukuzwa mpaka mbinguni? Hapana, utatupwa chini hadi mahali pa kifo.
16 Mtu yeyote akiwasikiliza ninyi wafuasi wangu, hakika ananisikiliza mimi. Lakini mtu yeyote akiwakataa ninyi, hakika ananikataa mimi. Na mtu yeyote akinikataa mimi anamkataa Yule aliyenituma.”
© 2017 Bible League International