Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Readings for Lent and Easter

Short readings from throughout the Bible that focus on the meaning and events of Easter.
Duration: 47 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
1 Petro 2:13-25

Tii Mamlaka Yote ya Kibinadamu

13 Nyenyekeeni kwa mamlaka yo yote ya kibinadamu kwa ajili ya Bwana. Mnyenyekeeni mfalme, aliye mamlaka ya juu kabisa. 14 Na muwatii viongozi waliotumwa na mfalme. Wametumwa ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale wanaofanya mazuri. 15 Kwa kuwa mapenzi ya Mungu ni kwamba, kwa kutenda mema mtayanyamazisha mazungumzo ya kijinga ya watu wasio na akili. 16 Muishi kama watu walio huru, lakini msiutumie uhuru huo kama udhuru wa kufanya maovu. Bali muishi kama watumishi wa Mungu. 17 Onesheni heshima kwa watu wote: Wapendeni ndugu zenu na dada zenu waliomo nyumbani mwake Mungu. Mcheni Mungu na mumheshimu mfalme.

Mfano wa Mateso ya Kristo

18 Watumwa mlio nyumbani, watumikieni mabwana wenu kwa heshima yote,[a] siyo tu wale walio wapole na wenye busara, bali hata wale walio wakali. 19 Baadhi yenu mtapata mateso wakati ambapo hamjafanya kosa lolote. Ikiwa utaweza kuvumilia maumivu na kuweka fikra zako kwa Mungu, hilo linampendeza sana Mungu. 20 Kwani kuna sifa gani iliyopo kwako kama utapigwa kwa kutenda mabaya na kuvumilia? Lakini kama utateseka kwa kutenda mema na kustahimili, hili lampendeza Mungu. 21 Ni kwa kusudi hili mliitwa na Mungu, kwa sababu Kristo pia aliteseka kwa ajili yenu na kwa kufanya hivyo aliacha kielelezo kwenu, ili tuweze kuzifuata nyayo zake.

22 “Hakutenda dhambi yo yote,
    wala hakukuwa na udanganyifu uliopatikana kinywani mwake.”(A)

23 Alipotukanwa hakurudishia matusi. Alipoteseka, hakuwatishia, bali wakati wote alijitoa mwenyewe kwa Mungu ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu kwenye mwili wake hadi pale msalabani, ili tuweze kuacha kuishi kwa ajili ya dhambi na kuishi kwa ajili ya haki. Ilikuwa ni kwa njia ya majeraha yake kwamba mliponywa. 25 Kwani mlikuwa kama kondoo wanaotangatanga huko na huko, lakini sasa mmerudi kwa Mchungaji na Mwangalizi wa maisha yenu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International