Old/New Testament
Neno Alifanyika Mwili
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: “Huyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu.
Ujumbe Wa Yohana Mbatizaji
19 Viongozi wa Wayahudi waliwatuma makuhani na Walawi wakam wulize Yohana, “Wewe ni nani?” 20 Yohana akawajibu wazi wazi pasipo kuficha, “Mimi siye Kristo.” 21 Wakamwuliza, “Wewe ni nani basi? Wewe ni Eliya ?” Akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.” 22 Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Tueleze, wewe hasa ni nani?”
23 Akawajibu kwa kutumia maneno ya nabii Isaya, “Mimi ni sauti ya mtu anayeita kwa sauti kuu nyikani, ‘Nyoosheni njia ata kayopita Bwana.”’ 24 Baadhi ya wale waliotumwa na Mafarisayo 25 walimwuliza, “Kama wewe si Kristo, wala Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini unabatiza watu?”
26 Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini kati yenu yupo mtu msiyemjua. 27 Yeye anakuja baada yangu, lakini mimi sistahili hata kumvua viatu vyake.”
28 Mambo haya yalitokea Bethania, kijiji kilichoko ng’ambo mashariki ya mto wa Yordani, ambapo Yohana alikuwa akibatiza watu.
Copyright © 1989 by Biblica