Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Lam for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Waebrania 10:19-39

Mkaribieni Mungu

19 Hivyo ndugu na dada, tuko huru kabisa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu. Tunaweza kufanya hivi bila hofu kwa sababu ya sadaka ya damu ya Yesu. 20 Tunaingia kwa njia mpya ambayo Yesu alitufungulia. Ni njia iliyo hai inayotuelekeza kupitia pazia; yaani mwili wa Yesu. 21 Na tunaye kuhani mkuu zaidi anayeisimamia nyumba ya Mungu. 22 Ikiwa imenyunyiziwa kwa damu ya Kristo, mioyo yetu imewekwa huru kutokana na dhamiri yenye hukumu, na miili yetu imeoshwa kwa maji safi. Hivyo mkaribieni Mungu kwa moyo safi, mkijaa ujasiri kwa sababu ya imani katika Kristo. 23 Tunapaswa kuling'ang'ania tumaini tulilonalo, bila kusitasita kuwaeleza watu juu yake. Tunaweza kumwamini Mungu kuwa atatimiza aliyoahidi.

Saidianeni Ninyi kwa Ninyi Kuwa Imara

24 Tunahitaji kumfikiria kila mtu kuona jinsi tunavyoweza kuhamasishana kuonesha upendo na kazi njema. 25 Tusiache kukutana pamoja, kama wanavyofanya wengine. Hapana, tunahitaji kuendelea kuhimizana wenyewe. Hili linazidi kuwa muhimu zaidi na zaidi kadri mnavyoona ile Siku inakaribia.

Msigeuke Mbali ya Mwana wa Mungu

26 Kama tutaamua kuendelea kutenda dhambi baada ya kujifunza ukweli, ndipo hakutakuwa sadaka nyingine itakayoondoa dhambi. 27 Tukiendelea kutenda dhambi, kitakachokuwa kimebaki kwetu ni wakati wa kutisha wa kuingoja hukumu na moto wa hasira utakaowaangamiza wale wanaoishi kinyume na Mungu. 28 Yeyote aliyekataa kuitii Sheria ya Musa alipatikana ana hatia kutokana na ushuhuda uliotolewa na mashahidi wawili au watatu. Watu wa jinsi hiyo hawakusamehewa. Waliuawa. 29 Hivyo fikiri jinsi watu watakavyostahili kuhukumiwa zaidi ambao wanaonesha kumchukia mwana wa Mungu; watu wanaoonesha kuwa hawana heshima kwa sadaka ya damu iliyoanzisha agano jipya na mara moja ikawatakasa au wale wanaomkashifu Roho wa neema ya Mungu. 30 Tunajua kuwa Mungu alisema, “Nitawaadhibu watu kwa ajili ya makosa wanayofanya”;(A) nitawalipa tu Pia alisema, “BWANA atawahukumu watu wake.”(B) 31 Ni jambo la kutiisha kukutana na hukumu kutoka kwa Mungu aliye hai.

Endeleeni na Ujasiri na Uvumilivu Mlionao

32 Zikumbukeni siku za kwanza mlipojifunza kweli. Mlikuwa na mashindano magumu pamoja na mateso mengi, lakini mkaendelea kuwa imara. 33 Mara zingine watu waliwasemea mambo ya chuki na kuwatesa hadharani. Na nyakati zingine mliwasaidia wengine waliokuwa wakitendewa vivyo hivyo. 34 Ndiyo, mliwasaidia magerezani na kushiriki katika mateso yao. Na bado mlikuwa na furaha wakati kila kitu mlichokimiliki kilipochukuliwa kutoka kwenu. Mkaendelea kufurahi, kwa sababu mlijua kwamba mnacho kitu kilicho bora zaidi; kitu kitakachoendelea milele.

35 Hivyo msipoteze ujasiri mliokuwa nao zamani. Ujasiri wenu utalipwa sana. 36 Mnahitajika kuwa na subira. Baada ya kufanya yale anayotaka Mungu, mtapata aliyowaahidi.

37 “Karibu sana sasa, yeye ajaye
    atakuja wala hatachelewa.
38 Mtu aliye sahihi mbele zangu
    ataishi akiniamini mimi.
Lakini sitafurahishwa na yule
    anayegeuka nyuma kwa ajili ya woga.”(C)

39 Lakini sisi siyo wale wanaogeuka nyuma na kuangamia. Hapana, sisi ni watu walio na imani na tunaokolewa.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International