Old/New Testament
20 Kwa imani Isaki aliwabariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yatakayotokea baadaye.
21 Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiegemea kichwa cha ile fimbo yake.
22 Kwa imani Yosefu alipokuwa amekaribia mwisho wa maisha yake, alitaja habari za kutoka kwa wana wa Israeli huko Misri, na akatoa maagizo kuhusu mifupa yake.
23 Kwa imani Mose alipozaliwa alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mwenye umbo zuri, wala hawakuogopa amri ya mfalme.
24 Kwa imani Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao, 25 badala yake akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu, kuliko kufurahia anasa za dhambi za kitambo kidogo. 26 Aliona kwamba kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni uta jiri mkubwa zaidi kuliko hazina ya Misri; maana alikuwa anataza mia kupata tuzo baadaye. 27 Kwa imani Mose alitoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme, kwa maana alivumilia kama amwonaye yeye asiyeonekana. 28 Kwa imani aliitimiza Pasaka na kunyunyiza damu ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.
29 Kwa imani watu wakavuka Bahari ya Shamu kama vile juu ya nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo, wakafa maji.
30 Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka, watu walipozizunguka kwa siku saba.
31 Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi.
32 Basi niseme nini zaidi? Wakati hauniruhusu kuwaeleza habari za Gidioni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii. 33 Hawa, kwa imani walishinda milki za wafalme, walite keleza haki, walipokea ahadi za Mungu, walifunga vinywa vya simba; 34 walizima moto mkali, na waliepuka kuuawa kwa upanga. Walikuwa dhaifu lakini wakatiwa nguvu, walikuwa hodari vitani, wakafukuza majeshi ya kigeni yakakimbia. 35 Wanawake walipokea wapendwa wao waliokuwa wamekufa wakafufuliwa. Lakini wengine wal iteswa wakakataa kufunguliwa, ili wapate kufufukia maisha bora zaidi. 36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata wakafungwa pingu na kutiwa gerezani. 37 Walipigwa mawe, walikatwa vipande viwili kwa misumeno, waliuawa kwa panga, walizurura wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, walikuwa maskini, waliteswa na kutendewa mabaya. 38 Ulimwengu haukustahili kuwa na watu kama hao: walizungukazunguka jangwani, katika milima na katika mapango na mashimo ardhini.
39 Na wote hawa, ingawa walishuhudiwa vema kwa sababu ya imani yao, hawakupokea yale waliyoahidiwa, 40 kwa sababu Mungu alikuwa amepanga kitu bora zaidi kwa ajili yetu, kwamba wasinge likamilishwa pasipo sisi.
Copyright © 1989 by Biblica