Old/New Testament
Dhabihu Ya Kristo Ilikuwa Ya Mwisho
10 Basi kwa kuwa sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo na wala si mambo yenyewe, haiwezi kamwe, kwa njia ya dhabihu zito lewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaoabudu. 2 Kama isingekuwa hivyo, dhabihu hizo zingekuwa hazitolewi tena. Maana hao waabuduo wasingalijiona tena kuwa wana hatia kwa ajili ya dhambi zao baada ya kutakaswa mara moja. 3 Badala yake, dhabihu hizo zilikuwa ni ukumbusho wa dhambi mwaka hadi mwaka. 4 Kwa maana damu ya mafahali na mbuzi, haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
5 Kwa sababu hii, Yesu alipokuja duniani alisema: “Hukutaka dhabihu na sadaka bali umeniandalia mwili. 6 Hukupendezwa na sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi. 7 Ndipo nikasema, ‘Nipo hapa, kama ilivyoandikwa katika gombo la sheria kunihusu; nimekuja kutimiza mapenzi yako wewe Mungu.’ ”
8 Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi hukutaka, wala huku pendezwa nazo,” ingawa hizi zilitolewa kwa mujibu wa sheria. 9 Kisha akasema, “Niko hapa, nimekuja kutimiza mapenzi yako.” Anaweka kando ule utaratibu wa kwanza na kuanzisha utaratibu wa pili. 10 Na kwa mapenzi hayo, sisi tumetakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu, kwa wakati wote.
11 Kila kuhani husimama siku hadi siku akifanya huduma yake ya ibada na akitoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kuondoa dhambi. 12 Lakini Kristo alipokwisha kutoa dhabihu yake kwa ajili ya dhambi mara moja tu kwa wakati wote, aliketi upande wa kulia wa Mungu. 13 Tangu wakati huo anangoja mpaka Mungu atakapowafanya maadui zake kuwa kiti cha miguu yake. 14 Maana kwa dhabihu moja tu amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
15 Roho Mtakatifu pia anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: 16 “Hili ndilo agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao na kuziandika akilini mwao.” 17 Kisha anasema: “Dhambi zao na makosa yao sitayakumbuka tena kamwe.”
18 Basi, haya yakishasamehewa, hakuna tena dhabihu inayoto lewa kwa ajili ya dhambi.
Copyright © 1989 by Biblica