Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Isa for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Waefeso 5:1-16

Kwa hiyo mfuateni Mungu kama watoto wapendwa. Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. Lakini uasherati, uchafu wa aina zote na tamaa, wala yasitajwe miongoni mwenu, kwa maana mambo haya hayawastahili watakatifu wa Mungu. Kusiwepo na mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuuzi au mzaha; mazungumzo ya namna hii hayafai. Badala yake mshukuruni Mungu. Mjue hakika kwamba hakuna mwasherati wala mtu mwenye mawazo machafu, wala mwenye tamaa, yaani mwabudu sanamu, ambaye ataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. Msikubali kudan ganywa na mtu ye yote kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya watu wote wasiomtii. Kwa hiyo, msishirikiane nao. Zamani ninyi pia mlikuwa gizani, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana; basi muishi kama watoto wa nuru. Kwa maana tunda la nuru hupatikana katika kila lililo jema, lililo la haki na la kweli. 10 Jifunzeni mambo yanayom pendeza Bwana. 11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofa a, bali yafichueni. 12 Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo wanayofanya kwa siri. 13 Lakini ikiwa jambo lo lote linawekwa katika nuru, huonekana, kwa maana ni nuru inayofanya vitu vionekane. 14 Ndio sababu husemwa, “Amka wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, na Kristo atakuangazia.” 15 Kwa hiyo muwe waangalifu jinsi mnavyoishi; msiishi kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima, 16 mkitumia vizuri muda mlio nao, kwa maana hizi ni nyakati za uovu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica