Old/New Testament
Paulo Anajivunia Mateso Yake
16 Nasema tena, mtu ye yote asidhani kwamba mimi ni mjinga. Lakini hata kama mkinidhania hivyo, basi nipokeeni kama mjinga ili nipate kujisifu kidogo. 17 Ninayosema sasa, kwa majivuno, nasema kama mjinga na wala si kwa mamlaka ya Bwana. 18 Kwa sababu wengine wanajivunia mambo ya kidunia, basi na mimi nitaji sifu. 19 Ninyi mnawavumilia wajinga kwa kuwa mna hekima mno! 20 Tena mnavumilia hata kama mtu anawafanya watumwa au anawany onya na kuwadanganya au anajigamba mbele yenu au anawapiga makofi usoni. 21 Naona aibu kukubali kwamba sisi ni wadhaifu kiasi ambacho hatuwezi kufanya mambo kama hayo. Lakini cho chote ambacho mtu anathubutu kujivunia, sasa nasema kama mjinga, mimi pia naweza kuthubutu kujivunia.
22 Je, wao ni Waebrania? Mimi pia ni Mwebrania. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. 23 Wao ni watumishi wa Kristo? Mimi ni mtumishi bora zaidi, nasema kama kichaa. Nimefanya kazi zaidi, nimefungwa gerezani zaidi, nimechapwa viboko visivyo na hesabu, na mara nyingi nilikuwa karibu kufa. 24 Mara tano nimechapwa viboko aro baini kupungua kimoja na Wayahudi. 25 Nimechapwa kwa chuma mara tatu. Nimepigwa mawe mara moja. Mara tatu nimevunjikiwa na meli. Nimeelea baharini usiku kucha na mchana kutwa. 26 Katika safari zangu nyingi, nimekuwa katika hatari za mafuriko, hatari za wany ang’anyi, hatari kutoka kwa Wayahudi wenzangu na hatari kutoka kwa watu wa mataifa mengine; nimekuwa katika hatari mijini, nyikani, baharini na katika hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. 27 Nimekuwa katika kazi ngumu na taabu, siku nyingi nimekuwa bila usingizi, nimekuwa na njaa na kiu, mara nyingi nimekuwa bila chakula, katika baridi na bila nguo. 28 Na ukiacha mambo mengine nimelemewa na wasiwasi juu ya makanisa yote. 29 Je, ni nani ana kuwa mdhaifu nisijisikie mdhaifu? Nani anashawishiwa kutenda dhambi nisijisikie nachomwa na uchungu?
30 Nikilazimika kujisifu, basi nitajisifia yale mambo yanay oonyesha udhaifu wangu. 31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye amebarikiwa daima, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. 32 Kule Dameski, gavana aliyekuwa chini ya Mfalme Areta aliu linda mji wa Dameski ili wapate kunikamata, 33 lakini nilish ushwa kwa kapu kubwa kupitia katika dirisha ukutani nikaepuka kukamatwa.
Copyright © 1989 by Biblica