Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
1 Wakorintho 15:29-58

29 Vinginevyo, kwa nini watu wanabatizwa kwa niaba ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa niaba yao? 30 Na kwa upande wetu kwa nini tunajitia hatarini kila wakati? 31 Nakufa kila siku, nasema kweli ndugu zangu, kama ninavyojivuna kwa ajili yenu katika Kristo Yesu, Bwana wetu. 32 Kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso kwa sababu za kibinadamu, nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, basi, “Tule na kunywa, kwa maana kesho tutakufa.” 33 Mtu asiwadanga nye, “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34 Pateni tena fahamu, muache kutenda dhambi. Kwa maana baadhi yenu hawam jui Mungu; nasema mambo haya ili muone aibu.

Ufufuo Wa Mwili

35 Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wanafufuliwaje? Wata kuwa na mwili wa namna gani?” 36 Wapumbavu ninyi! Mnachopanda hakiwi hai tena kama hakikufa. 37 Unapopanda, hupandi mwili unaoutegemea, bali unapanda mbegu, pengine mbegu ya ngano au ya nafaka nyingine. 38 Lakini Mungu huipa hiyo mbegu umbo kama alivyochagua mwenyewe, na kila aina ya mbegu ina umbo lake. 39 Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine na hali kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40 Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani; lakini uzuri wa miili ya mbinguni ni wa aina moja na uzuri wa miili ya duniani ni wa aina nyingine. 41 Jua lina uzuri wa aina moja, mwezi nao una uzuri wake na nyota pia; na nyota hutofautiana na nyota nyingine kwa uzuri.

42 Ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Mwili uliopandwa ni wakuharibika; utafufuliwa usioharibika; 43 unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu; unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu. 44 Unapandwa ukiwa mwili wa asili, unafufuliwa ukiwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 45 Kwa hiyo imeandikwa, “Adamu wa kwanza akawa kiumbe hai,” Adamu wa mwisho akawa roho inayohuisha. 46 Lakini si yule wa kiroho aliyekuja kwanza; bali ni yule wa mwili, na kisha yule wa kiroho. 47 Mtu wa kwanza alitokana na mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48 Na kama alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na alivyo mtu wa mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyochukua umbile la mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua umbile la yule mtu kutoka mbinguni. 50 Nawatangazia ndugu zangu kwamba nyama na damu haviwezi kurithi Ufalme wa Mungu, wala uharibifu hauwezi kurithi kutokuharibika.

51 Sikilizeni, nawaambia siri: sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52 ghafla, kufumba na kufumbua, tarumbeta ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa tarumbeta italia, wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53 Kwa maana hali hii ya kuharibika lazima ivae kutokuharibika, na hali hii ya kufa lazima ivae hali ya kutokufa. 54 Kwa hiyo, wakati kuharibika kutakapovaa kutokuharibika, na mwili wa kufa utakapovaa hali ya kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia, “Kifo kimemezwa na ushindi .” 55 “Mauti, ushindi wako uko wapi? Na uchungu wako uko wapi?” 56 Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 Lakini, Mungu ashukuriwe! Yeye anatupa tia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

58 Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica