Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
1 Wakorintho 11:1-16

Utaratibu Wa Kuabudu

11 Niigeni mimi, kama mimi ninavyomuiga Kristo. Ninawasifu kwa sababu mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kuwa mnashika mafundisho niliyowakabidhi. Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. Kwa hiyo mwanamume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anaaib isha kichwa chake. Na mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anaaibisha kichwa chake, ni sawa kama ame nyoa nywele zote kichwani. Kama mwanamke hataki kufunika kichwa chake, nywele zake zinyolewe; na kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa kichwa chake, au kukata nywele zake, basi afunike kichwa chake. Mwanamume asifunike kichwa chake kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. Kwa maana mwanamume hakuumbwa kutoka kwa mwanamke, bali mwanamke ame toka kwa mwanamume. Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwa namke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume. 10 Hii ndio sababu inampasa mwanamke afunike kichwa chake na kwa ajili ya malaika. 11 Lakini katika Bwana mwanamke hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamume, wala mwanamume hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamke. 12 Kwa maana kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanamume, vivyo hivyo sasa mwanamume anazaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vinatoka kwa Mungu.

13 Amueni wenyewe, je, ni sawa kwa mwanamke kumwomba Mungu akiwa hakufunika kichwa chake? 14 Je, maumbile ya asili hayatu fundishi kuwa ni aibu kwa mwanamume kuwa na nywele ndefu? 15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni sifa kwake. Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu za kumfunika. 16 Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica