Old/New Testament
19 Je, nikisema hivyo nina taka kusema kwamba sadaka iliyotolewa kwa sanamu au kwamba sanamu ina maana yo yote? 20 La, sivyo. Lakini sadaka inayotolewa kwa sanamu inatolewa kwa mashetani, na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muwe na ushirika na mashetani. 21 Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na kunywa katika kikombe cha mashetani pia. Hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya mashe tani. 22 Je, tunataka kujaribu kumfanya Bwana awe na wivu? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?
Uhuru Wa Mwamini
23 Vitu vyote vinaruhusiwa, lakini si vitu vyote vina faida. ‘Vitu vyote ni halali,’ lakini si vyote vinajenga. 24 Mtu asita fute yale yanayomfaa yeye peke yake, bali atafute yale yanayomfaa jirani yake.
25 Kuleni cho chote kinachouzwa katika masoko ya nyama bila kuuliza maswali kuhusu dhamiri. 26 Kwa maana, ‘Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.’ 27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kitakachokuwa mezani bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama ukiam biwa, “Hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu,” basi kwa ajili ya huyo aliyekuambia juu ya hicho chakula, na kwa ajili ya dhamiri, usile. 29 Namaanisha dhamiri ya huyo aliyekuambia, si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30 Kama nakula kwa shukrani, kwa nini nashutu miwa kwa kile ambacho ninatoa shukrani?
31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kik wazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki, au kwa kanisa la Mungu; 33 kama mimi ninavyojaribu kumridhisha kila mtu katika kila kitu ninachofanya. Kwa maana sitafuti kujiridhisha mwenyewe bali nata futa faida ya walio wengi, ili waweze kuokolewa.
Copyright © 1989 by Biblica