Old/New Testament
20 Kila mtu abaki katika nafasi ambayo alikuwa nayo alipoitwa kuamini. 21 Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Lakini kama unaweza kuwa huru, utumie nafasi hiyo. 22 Kwa maana aliyeitwa kwa Bwana akiwa mtumwa ni mtu huru wa Bwana. Hali kadhalika mtu aliyekuwa huru alipoitwa ni mtumwa wa Kristo. 23 Mmenunuliwa kwa gharama; msikubali kuwa watumwa wa watu. 24 Kwa hiyo ndugu zangu, kila mmoja wenu akae na Mungu katika nafasi aliyokuwa nayo alipoitwa.
Kwa Hali Ya Sasa, Afadhali Kutokuoa
25 Sasa, kuhusu wale walio bikira. Sina amri yo yote kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa ushauri kama mtu aliyemwaminifu kwa rehema ya Bwana.
26 Kwa sababu ya dhiki iliyopo, nadhani itakuwa vyema mki baki kama mlivyo. 27 Je, umeoa? Basi usitake talaka. Kama hujaoa usitafute mke. 28 Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa hajatenda dhambi. Lakini wanaooa watakabil iana na matatizo mengi katika maisha haya, nami ningependa myaep uke kwa kubaki mlivyo.
29 Nikisema hivyo ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa waliooa waishi kama hawakuoa; 30 na wana oomboleza kama hawaoombolezi; wenye furaha kama hawana furaha; wanaonunua kama walivyonunua si mali yao; 31 na wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inatoweka.
32 Ningependa msiwe na wasiwasi. Mwanamume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza. 33 Lakini mwanamume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi ya kumfurahisha mke wake. 34 Kwa sababu hiyo, ana vutwa huku na huko. Mwanamke asiyeolewa au msichana bikira anaj ishughulisha na kazi ya Bwana, jinsi ya kuwa mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini mwanamke aliyeolewa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mume wake. 35 Ninasema haya kwa faida yenu na sio kuwawekea vikwazo. Napenda muishi sawa na kumpa Bwana maisha yenu yote. 36 Kama mtu anafikiri kwamba mwenendo wake kwa mchumba wake si sawa, na hasa kama mchumba wake anaanza kuzeeka, na anaona anawajibika kumuoa, basi afanye anavyoona vyema; waoane, si dhambi. 37 Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake. 38 Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.
39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana. 40 Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.
Copyright © 1989 by Biblica