Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Warumi 11:1-18

Huruma Ya Mungu Kwa Waisraeli

11 Kwa hiyo nauliza, je, Mungu amewakataa watu wake? La, sivyo. Mimi mwenyewe ni Mwisraeli, wa uzao wa Ibrahimu na wa kabila la Benjamini. Mungu hajawakataa watu wake ambao aliwajua tokea mwanzo. Hamfahamu Maandiko yanavyosema kuhusu Eliya, jinsi alivyomlalamikia Mungu kuhusu Waisraeli akisema, “Bwana, wamewaua manabii wako na kuziharibu madhabahu zako, nimebaki mimi peke yangu, nao wanataka kuniua? Na Mungu alimjibuje? “Nime bakiza kwa ajili yangu watu elfu saba ambao hawajapiga magoti kumwabudu Baali.” Ndivyo ilivyo hata sasa; wapo wachache wal iosalia ambao Mungu amewachagua kwa neema yake. Lakini ikiwa wamechaguliwa kwa neema, haiwezekani tena wakachaguliwa kwa msingi wa matendo. Kama ingekuwa hivyo, neema isingekuwa neema tena.

Tusemeje basi? Waisraeli walishindwa kupata kile ambacho walikitafutakwa bidii. Lakini waliochaguliwa walikipata. Wa liobaki walifanywa wagumu, kama Maandiko yasemavyo, “Mungu ali wapa mioyo mizito, na macho ambayo hayawezi kuona, na masikio ambayo hayawezi kusikia, hata mpaka leo.” Naye Daudi anasema: “Karamu zao na ziwe mtego wa kuwanasa, na kitu cha kuwakwaza waanguke na kuadhibiwa, 10 Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona, na migongo yao ipinde kwa taabu daima.”

Kurejeshwa Kwa Waisraeli

11 Nauliza tena, je, Waisraeli walipojikwaa walianguka na kuangamia kabisa? La sivyo! Lakini kwa sababu ya uhalifu wao, wokovu umewafikia watu wa mataifa mengine, ili Waisraeli waone wivu. 12 Ikiwa uhalifu wao umeleta utajiri mkubwa kwa ulimwe ngu, na kama kuanguka kwao kumeleta utajiri kwa watu wasiomjua Mungu, basi Waisraeli wote watakapoongoka itakuwa ni baraka kub wa zaidi.

13 Sasa ninasema nanyi watu wa mataifa mengine. Mimi ni mtume kwa watu wa mataifa na ninajivunia huduma hiyo 14 ili kuwafanya Wayahudi wenzangu waone wivu, na hivyo niwaokoe baadhi yao. 15 Kwa kuwa ikiwa kukataliwa kwao kumefanya ulimwengu wote upatanishwe na Mungu, kuokolewa kwao je, si kutakuwa ni uhai kutoka kwa wafu? 16 Na kama sehemu ya kwanza ya unga ulioumuliwa ni wakfu, basi unga wote ni wakfu; na kama shina ni wakfu, matawi nayo yatakuwa wakfu.

17 Lakini kama baadhi ya matawi yamekatwa, na ninyi kama mizeituni mwitu mkapandwa katika shina, mkashiriki pamoja na matawi mengine chakula kutoka katika shina la mzeituni, 18 msi jivune mbele ya hayo matawi. Kama mkijisifu mkumbuke kuwa si ninyi mnaoshikilia shina, bali ni shina linalowashikilia ninyi.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica