Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Warumi 8:22-39

22 Tunajua kwamba mpaka sasa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa uchungu mkali kama ule wa uzazi. 23 Na si hivyo tu, hata sisi ambao tuna matunda ya kwanza ya Roho tunalia kwa uchungu tukisu biri kwa hamu kufanywa kuwa wana wa Mungu, miili yetu itakapowek wa huru kabisa.

24 Kwa maana tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alichonacho? 25 Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatunacho, basi tunakingoja kwa subira.

26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na mapenzi ya Mungu. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya hivyo kwa faida yao. 29 Wale ambao Mungu alikwisha kuwachagua tangu mwanzo, pia aliwateua wafanane na Mwanae, ili Mwana awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale ambao Mungu aliwateua tangu awali pia ali waita; na wale aliowaita pia aliwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki aliwapa utukufu wake.

Upendo Wa Mungu

31 Tuseme nini basi kuhusu haya yote? Ikiwa Mungu yuko upande wetu ni nani atakayetupinga? 32 Ikiwa Mungu hakumwacha Mwanae bali alimtoa kwa ajili yetu sote, hatatupatia pamoja na Mwanae, vitu vyote? 33 Ni nani atawashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ambaye anawahesabia kuwa hawana hatia. 34 Ni nani basi atakayewahukumu? Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyekufa, na zaidi ya hayo, yeye ndiye aliyefufuliwa akawa hai, na ambaye sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, naye anatuombea. 35 Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo? Ni shida? Au taabu? Au mateso? Au njaa? Au umaskini? Au hatari? Au Kifo? Hapana. 36 Kama Maandiko yasemavyo: “Kwa aji li yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.” 37 Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda. 38 Kwa maana nina hakika kuwa, si kifo wala uzima; si malaika wala mashetani; si mambo ya sasa wala mambo yajayo au mamlaka nyingineyo yote; 39 si mambo yaliyo juu wala yaliyo chi ni sana; wala hakuna kitu kingine cho chote kati ya vitu vyote alivyoumba Mungu kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica