Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 23:1-15

23 Paulo akawakazia macho wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, mimi nimeishi nikiwa na dhamiri safi kabisa siku zote mbele za Mungu, mpaka leo.” Kuhani mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi mdomoni. Ndipo Paulo akasema, “Mungu atakupiga, wewe ukuta uliopakwa chokaa! Unawe zaje kusikiliza kesi hii kwa mujibu wa sheria, na hapo hapo, kinyume cha sheria, unaamuru nipigwe?” Wale watu waliokuwa wamesimama karibu wakamwambia Paulo, “Mbona unamtukana kuhani mkuu wa Mungu?” Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye ni kuhani mkuu. Kwa maana Maandiko yanasema, ‘Usimseme vibaya kiongozi wa watu wako.’ ” Paulo alipotambua ya kuwa baadhi ya wajumbe wa baraza walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo alisema nao kwa sauti kubwa, “Ndugu zangu! Mimi ni Mfarisayo, mtoto wa Mafarisayo; na hapa nimeshitakiwa kuhusu tumaini juu ya ufufuo wa wafu.” Aliposema haya, Mafarisayo na Masadukayo wakafarakana na baraza zima likagawanyika. Kwa maana Masadukayo wanaamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho; lakini Mafarisayo wanaamini haya yote. Kelele zikazidi sana; na baadhi ya waandishi wa sheria wa upande wa Mafarisayo, wakasimama wakiwapinga wengine wakasema, “Hatuoni kosa lo lote alilofanya mtu huyu! Huenda ikawa malaika au roho amezungumza naye kweli!” 10 Mabishano yalipozidi kuwa makali, yule jemadari aliogopa kuwa wangeweza kumrarua Paulo vipande vipande. Kwa hiyo akaamuru askari wakamtoe Paulo alipokuwa, arudishwe kwenye ngome ya jeshi. 11 Usiku uliofuata, Bwana akamtokea Paulo akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, itakubidi unishuhudie na huko Rumi pia.”

Njama Za Wayahudi Kumwua Paulo

12 Kulipopambazuka Wayahudi wakala njama ya kumwua Paulo. Wakaweka nadhiri kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamemwua Paulo. 13 Waliofanya mpango huu walikuwa zaidi ya watu arobaini. 14 Wakaenda kwa kuhani mkuu na wazee wakasema, “Tumeweka nad hiri ya pamoja kwamba hatutakula wala kunywa mpaka tumwue Paulo. 15 Kwa hiyo ninyi pamoja na baraza, pelekeni ombi kwa jemadari ili Paulo aletwe barazani, mtoe udhuru kwamba mnataka kuchunguza kesi yake kwa usahihi zaidi. Sisi tutakuwa tayari kumwua hata kabla hajakaribia kufika hapa.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica