Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Job for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 7:44-60

44 “Baba zetu walikuwa na ile hema ya ushuhuda pamoja nao jangwani. Nayo ilikuwa imetengenezwa kama malaika alivyomwelekeza Musa itengenezwe; na kwa mshono ambao Musa alikuwa ameonyeshwa. 45 Nao baba zetu wakaileta hiyo hema wakiongozwa na Yoshua wali poiteka nchi kutoka kwa yale mataifa ambayo Mungu aliyafukuza mbele yao. Na hivi ndivyo ilivyokuwa mpaka wakati wa mfalme Daudi 46 ambaye alipendwa na Mungu, naye akaomba apewe ruhusa amjengee Mungu wa Yakobo makao. 47 Lakini mfalme Sulemani ndiye aliyem jengea Mungu nyumba. 48 Hata hivyo Mungu aliye Mkuu sana hakai kwenye nyumba iliyojengwa kwa mikono na binadamu. Kama nabii alivyosema, 49 ‘Mbingu ni kiti changu cha Enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu: mtanijengea nyumba ya namna gani? Auliza Bwana. Au mahali pangu pa kupumzikia ni wapi? 50 Je, si mimi niliyeumba vitu vyote hivi?’

51 “Ninyi watu wenye shingo ngumu! Wenye mioyo ya kipagani! Mmekuwa viziwi kwa neno la Mungu wala hamchoki kumpinga Roho Mta katifu! Kama walivyofanya baba zetu nanyi leo mnafanya vivyo hivyo. 52 Je, kuna nabii hata mmoja ambaye baba zetu hawa kumtesa? Waliwaua hata wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki, ambaye ninyi mmemsaliti kisha mkamwua. 53 Ninyi mlizipokea sheria za Mungu zilizoletwa kwenu na malaika lakini hamkuzitii.”

Stefano Auawa Kwa Kupigwa Mawe

54 Basi wale viongozi waliposikia maneno haya walijawa na hasira, wakasaga meno yao kwa ghadhabu. 55 Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, akamwona Yesu amesimama upande wa kulia wa Mungu.” 56 Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

57 Wao wakapiga makelele, wakaziba masikio yao wasimsikie, wakamrukia kwa pamoja. 58 Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Na mashahidi walioteuliwa walimwachia kijana mmoja aitwae Sauli mavazi yao. 59 Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, Bwana Yesu, pokea roho yangu!” 60 Akapiga magoti akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema haya, akafa.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica