Old/New Testament
22 Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri akawa mtu shujaa kwa maneno na matendo yake. 23 Musa alipokuwa na umri wa miaka arobaini akawa na hamu ya kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. 24 Alipoona mmoja wao akionewa na Mmisri, akamwua yule Mmisri kulipiza kisasi. 25 Alidhani kuwa ndugu zake wangeelewa kwamba Mungu ali kuwa akiwaokoa kwa msaada wake, lakini wao hawakuelewa. 26 Kwa hiyo siku ya pili alipoona Waisraeli wanagombana alijaribu kuwa patanisha, akawaambia, ‘Jamani, ninyi ni ndugu. Mbona mnaoneana wenyewe kwa wenyewe?’ 27 Lakini yule aliyekuwa akimwonea mwen zake akamsukumia Musa kando, akamwuliza, ‘Ni nani aliyekuweka uwe mtawala na mwamuzi kati yetu? 28 Je, unataka kuniua kama ulivy omwua yule Mmisri jana?’ 29 Musa aliposikia maneno haya alikim bia akatoka Misri akaenda kuishi kama mkimbizi sehemu za Midiani. Huko akawa baba wa watoto wawili wa kiume. 30 “Baada ya miaka arobaini, malaika wa Mungu akamtokea jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kina waka moto. 31 Musa alishangazwa na kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto; na aliposogea karibu ili aone vizuri, akasikia sauti ya Bwana ikisema, 32 ‘Mimi ni Mungu wa baba zako; Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka na wa Yakobo.’ Musa alitetemeka kwa hofu akaogopa kutazama.
33 “Mungu akamwambia, ‘Vua viatu vyako kwa maana hapo uli posimama ni mahali patakatifu. 34 Nimeona mateso ya watu wangu walioko Misri, na nimesikia kilio chao, nami nimeshuka ili niwaokoe. Basi sasa nitakutuma Misri.’ 35 Huyu Musa ndiye wali yemkataa wakisema, ‘Ni nani aliyekufanya uwe mtawala na mwamuzi wetu?’ Mungu alimtuma kama mtawala na mkombozi kwa njia ya yule malaika aliyemtokea katika kile kichaka. 36 Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya maajabu na ishara nyingi huko Misri na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.
37 “Huyu Musa ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, ‘Mungu atawateulia nabii kutoka miongoni mwa ndugu zenu kama alivyoni teua mimi.’ 38 Huyu Musa alikuwa katika kusanyiko la wana wa Israeli jangwani pamoja na baba zetu na yule malaika aliyezun gumza naye kwenye Mlima wa Sinai; akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.
39 “Lakini baba zetu walikataa kumtii Musa, wakamsusia, na mioyoni mwao wakarudi Misri. 40 Wakamwambia Haruni, ‘Tufanyie miungu watakaotuongoza; kwa maana huyu Musa aliyetutoa Misri hat ujui yaliyompata.’ 41 Siku hizo wakatengeneza kinyago mfano wa ndama, wakakitolea sadaka za kuteketezwa, kisha wakafanya sherehe kushangilia kitu walichotengeneza kwa mikono yao wenyewe. 42 Ndipo Mungu akaondoka kati yao, akawaacha waabudu sayari za angani kama miungu yao: jua, mwezi na nyota. Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, ‘ Je, nyumba ya Israeli, mlinitolea sadaka za wanyama wa kuteketezwa kwa miaka arobaini jangwani? La! 43 Tazama mlibeba hema ya Moleki, na sanamu ya nyota wa Refani, miungu mliyotengeneza ili muiabudu. Kwa hiyo nitawapeleka utum wani, mbali kuliko Babiloni.’
Copyright © 1989 by Biblica