Old/New Testament
22 Lakini wale maafisa wal iotumwa walipoingia gerezani hawakuwakuta wale mitume mle. Kwa hiyo wakarudi kutoa ripoti kwa baraza. 23 Wakasema, “Tumekuta milango ya jela imefungwa sawasawa, na maaskari wa gereza wamesi mama nje ya milango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu ye yote ndani.”
24 Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia ripoti hiyo wakashangaa sana wasijue mambo haya yan geishia wapi. 25 Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Wale watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.”
26 Ndipo yule mkuu wa kikosi cha walinzi wa Hekalu na wale maofisa wakaenda wakawaleta mitume lakini hawakuwadhuru kwa sababu waliogopa wangelipigwa mawe na watu. 27 Baada ya kuwaleta wakawaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu akaanza kuwahoji,
28 “Tuliwakanya msifundishe kwa jina la huyu mtu, lakini ninyi mmeeneza mafundisho yenu Yerusalemu yote, na tena mmeamua kuwa sisi tuna hatia juu ya kifo chake.”
29 Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu na sio wanadamu. 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu ambaye ninyi mlimwua kwa kumtundika kwenye msalaba. 31 Mungu alimwinua, akamweka mkono wake wa kuume awe Mtawala na Mwokozi ili awape wana wa Israeli toba na msamaha wa dhambi. 32 Nasi tu mashahidi wa mambo haya pamoja na Roho Mtakatifu aliyetolewa na Mungu kwa watu wanaomtii.”
Mungu kwa watu wanaomtii.”
33 Wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua wale mitume. 34 Lakini mmoja wao, Far isayo aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa sheria aliyeh eshimiwa na watu wote, akasimama akaamuru wale mitume watolewe nje kwa muda.
35 Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Wazee wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mtakalowatendea watu hawa! 36 Kumbukeni kuwa sio zamani sana tangu alipotokea mtu aliyeitwa Theuda ambaye alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi mia nne wal ioambatana naye. Lakini aliuawa na wafuasi wake wote wakatawany ika, kazi yake ikawa bure. 37 “Baada yake alitokea Yuda Mgali laya wakati ule wa sensa, akapata wafuasi wengi; lakini naye akauawa nalo kundi lake likatawanyika.
38 “Kwa hiyo, kwa kesi hii nawashauri waacheni watu hawa wala msiwatendee lo lote, kwa maana kama mpango wao na kazi yao ni mambo ya wanadamu hayatafika po pote; 39 lakini ikiwa ni kazi ya Mungu hamtaweza kuwazuia. Badala yake huenda mkajikuta mnam pinga Mungu!”
40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli; wakawaita mitume ndani na baada ya kuwachapa viboko wakawaamuru wasifundishe kwa jina la Yesu. Wakawaachia waende zao. 41 Wale mitume walitoka barazani wamejaa furaha kwa sababu Mungu aliwapa heshima ya kupata aibu ya kuchapwa viboko kwa ajili ya jina la Yesu. 42 Na kila siku Hek aluni na nyumbani walizidi kuhubiri na kufundisha bila kukoma, juu ya Habari Njema kwamba Yesu ndiye Kristo.
Copyright © 1989 by Biblica