Old/New Testament
Anania Na Safira
5 Pia mtu mmoja jina lake Anania na mkewe Safira waliuza mali yao. 2 Lakini Anania, kwa makubaliano na mkewe akaficha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobakia kwa mitume.
3 Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? 4 Kabla hujauza hilo shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza , fedha ulizopata zilikuwa zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”
Ujue hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”
5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini akafa. Na wote waliosikia maneno haya wakajawa na hofu. 6 Vijana wakaingia wakaufunga mwili wake wakamchukua nje kumzika.
7 Na baada ya muda wa saa tatu mkewe Anania akaingia, naye hakuwa na habari ya mambo yaliyotokea. 8 Petro akamwuliza, “Niambie, je? Mliuza shamba lenu kwa kiasi hiki?” Akajibu, “Ndio, tuliuza kwa kiasi hicho.”
9 Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje wewe na mumeo mkaamua kumjaribu Roho Mtakatifu wa Bwana? Tazama, vijana waliomzika mumeo wako mlangoni nao watakuchukua nje.”
10 Na mara akaanguka chini akafa. Wale vijana walipoingia wakamwona kuwa amekufa, wakamchukua wakamzika karibu na mumewe. 11 Waamini wote na watu wote waliosikia habari hizi wakajawa na hofu kuu.
Mitume Wafanya Miujiza Mingi Na Maajabu
12 Mitume walifanya miujiza mingi na ishara za ajabu. Na waamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Sulemani. 13 Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kujiunga nao lakini watu wote waliwaheshimu sana. 14 Hata hivyo watu wengi zaidi, wanaume kwa wanawake walikuwa wakiongezeka katika kundi la waliomwamini Bwana. 15 Hata walikuwa wakiwabeba wagonjwa wakawalaza kwenye mikeka barabarani ili Petro alipokuwa akipita kivuli chake kiwa guse angalau baadhi yao, wapone. 16 Pia watu walikusanyika kutoka katika miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu wakileta wagonjwa na watu waliopagawa na pepo wachafu, hao wote wakapo nywa.
Mitume Washitakiwa
17 Kuhani mkuu na wale waliomuunga mkono, yaani Masadukayo, walijawa na wivu, 18 wakawakamata mitume na kuwatia gerezani.
19 Lakini usiku ule malaika wa Bwana akaja akawafungulia milango ya gereza akawatoa nje akawaambia, 20 “Nendeni mkasi mame Hekaluni mkawaambie watu habari za maisha haya mapya!”
21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaanza kufundisha watu. Kuhani Mkuu alipowasili pamoja na wenzake wakaitisha mkutano wa baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani.
Copyright © 1989 by Biblica