Old/New Testament
Mavazi Ya Yesu Yagawanywa
23 Maaskari walipokwisha msulubisha Yesu, walichukua mavazi yake wakayagawa mafungu manne; kila askari akapata moja. Ila wal ikubaliana wasipasue ile kanzu yake kwa maana ilikuwa imefumwa tangu juu hadi chini na haikukatwa mahali po pote. 24 Wakaam biana, “Tusiipasue ila tupige kura tuone ni nani aichukue.” Hii ilitimiza yale Maandiko yaliyosema, “Waligawana mavazi yangu, na kanzu yangu wakaipigia kura.” 25 Kwa hiyo wakapiga kura. Karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Mariamu mama yake, shan gazi yake, Mariamu mke wa Klopa na Mariamu Magdalena. 26 Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, huyo ni mwanao!” 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Na huyo ni mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.
Kifo Cha Yesu
28 Baada ya haya Yesu alifahamu ya kuwa mambo yote yameka milika, kwa hiyo, ili kutimiza Maandiko, akasema, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo wakampandishia mdomoni. 30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.
31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani. 32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji. 35 Mambo haya yamehakikishwa na mtu aliyeyaona, na ushahidi wake ni wa kuaminika. Yeye anajua ya kuwa aliyosema ni kweli, naye ametoa ushuhuda huu ili nanyi mpate kuamini. 36 Kwa maana mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Na pia Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.” 38 Baada ya haya, Yusufu wa Arimathea aliyekuwa mfuasi wa siri wa Yesu, maana aliwaogopa Wayahudi, akamwomba Pilato auchukue mwili wa Yesu; naye akamruhusu. Kwa hiyo akaja, akauchukua mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye alimwen dea Yesu kwa siri usiku, alikuja na mchanganyiko wa manukato zaidi ya kilo thelathini. 40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakau vika sanda iliyokuwa na manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Way ahudi. 41 Karibu na pale walipomsulubisha palikuwa na bustani yenye kaburi ambalo lilikuwa halijatumika. 42 Kwa hiyo ili kuka milisha mazishi kabla ya sabato, wakamzika Yesu kwenye hilo kab uri lililokuwa karibu.
Copyright © 1989 by Biblica