Old/New Testament
Yesu Akamatwa
18 Baada ya sala hii Yesu aliondoka na wanafunzi wake waka vuka kijito cha Kidroni wakaingia katika bustani iliyokuwa upande wa pili. 2 Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, pia alipafahamu mahali hapo kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake hapo mara kwa mara. 3 Kwa hiyo Yuda akaja kwenye bustani hiyo akiongoza kikundi cha askari wa Kirumi na walinzi wa Hekalu kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo wakiwa na taa na silaha. 4 Yesu alijua yata kayompata, kwa hiyo akawasogelea akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5 Wao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti.” Yesu akawaambia, “Ni mimi.” Yuda ambaye alimsaliti alikuwa amesimama na wale askari. 6 Yesu alipowaambia, ‘Ni mimi,’ walirudi nyuma wakaanguka chini! 7 Akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Nao wakajibu, “Yesu wa Nazareti .” 8 Yesu akawaambia, “Nimekwisha waeleza kuwa ni mimi; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi waachilieni hawa wengine waende.” 9 Alisema haya ili lile neno alilosema lipate kutimia, ‘Kati ya wale ulionipa sikupoteza hata mmoja.’ 10 Ndipo Simoni Petro akachomoa upanga aliokuwa amechukua akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Jina la mtumishi huyo lilikuwa Malko. 11 Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala. Je, nisinywe kikombe cha mateso alichonipa Baba?” 12 Kwa hiyo mkuu wa kikosi na askari wake pamoja na wale walinzi wa Hekalu waliot umwa na viongozi wa Wayahudi, wakamkamata Yesu wakamfunga mikono. 13 Kisha wakampeleka kwanza kwa Anasi mkwewe Kayafa ambaye ali kuwa ndiye kuhani mkuu mwaka ule. 14 Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri viongozi wengine wa Kiyahudi kwamba ingekuwa afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Petro Anamkana Yesu
15 Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyu mwanafunzi mwingine alikuwa anafahamika kwa kuhani mkuu kwa hiyo aliingia ndani ya ukumbi pamoja na Yesu. 16 Lakini Petro alisimama nje karibu na mlango. Ndipo yule mwanafunzi mwin gine akazungumza na msichana aliyekuwa analinda mlangoni, akamru husu amwingize Petro ndani. 17 Yule msichana akamwuliza Petro, “Je, wewe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro aka jibu, “Hata! Mimi sio.” 18 Wale watumishi na askari walikuwa wamesimama wakiota moto wa mkaa ambao walikuwa wamewasha kwa sababu pale ukumbini palikuwa na baridi kali. Petro naye alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
Copyright © 1989 by Biblica