Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 11:30-57

30 Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini. Alikuwa bado yuko pale Martha alipokutana naye. 31 Wale Wayahudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walipoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwa hiyo wakamfuata. 32 Mariamu alipomwona Yesu aliinama chini kwa heshima akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu han galikufa.” 33 Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni; 34 akau liza, “Mmemzika wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.” 35 Yesu akalia. 36 Wale Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!” 37 Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwa nini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”

Yesu Amfufua Lazaro

38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe. 39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.” 40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. 42 Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.” 43 Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!” 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!”

Mpango Wa Kumwua Yesu

45 Wayahudi wengi waliokuja kumfariji Mariamu, walipoona yaliyotokea wakamwamini Yesu. 46 Lakini wengine walikwenda kwa Mafarisayo wakawaambia mambo Yesu aliyofanya. 47 Kwa hiyo maku hani wakuu na Mafarisayo wakafanya baraza wakaulizana, “Tufa nyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48 Kama tukimruhusu aendelee hivi, kila mtu atamwamini; na Warumi watakuja kuharibu Hekalu letu na taifa letu.” 49 Lakini mmoja wao, aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu kwa mwaka ule akawaambia wen zake, “Ninyi hamjui kitu! 50 Hamwoni kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, badala ya taifa lote kuangamia?” 51 Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka ule, alikuwa anatabiri kuwa Yesu angekufa kwa ajili ya Wayahudi; 52 na pia kwa ajili ya watoto wa Mungu wal iotawanyika ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53 Tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi wakawa wanafanya mipango ili wamwue Yesu. 54 Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani, bali alitoka Bethania akaenda mikoani karibu na jangwa, kwenye kijiji kimoja kiitwacho Efraimu. Alikaa huko na wanafunzi wake.

55 Wakati Pasaka ya Wayahudi ilipokaribia, watu wengi wali toka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajita kase kabla ya sikukuu. 56 Watu walikuwa wakimtafuta Yesu, wakawa wanaulizana wakati wamesimama Hekaluni, “Mnaonaje? Mnadhani ata kuja kwenye sikukuu?” 57 Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa kama yupo mtu anayefahamu alipo awafahamisha, ili wapate kumkamata.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica