Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Kgs for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 3:19-36

19 Na hukumu yenyewe ni kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu. 20 Kwa kuwa kila mtu atendaye maovu huchu kia nuru, wala hapendi kuja kwenye nuru ili matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini kila mtu anayeishi maisha ya uaminifu huja kwenye nuru, kusudi iwe wazi kwamba matendo yake yanatokana na utii kwa Mungu.”

Yesu Na Yohana Mbatizaji

22 Baadaye, Yesu alikwenda katika jimbo la Yudea pamoja na wanafunzi wake akakaa nao kwa muda na pia akabatiza watu. 23 Yohana naye alikuwa akibatiza watu huko Ainoni karibu na Sal imu kwa sababu huko kulikuwa na maji mengi. Watu walikuwa wakim fuata huko naye akawabatiza. 24 Wakati huo Yohana alikuwa bado hajafungwa gerezani.

25 Ukazuka ubishi kati ya wanafunzi kadhaa wa Yohana na Myahudi mmoja kuhusu swala la kutawadha. 26 Basi wakamwendea Yohana wakamwambia, “Rabi, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe nga’mbo ya pili ya mto wa Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!” 27 Yohana akawa jibu, “Mtu hawezi kuwa na kitu kama hakupewa na Mungu. 28 Ninyi wenyewe ni mashahidi wangu kwamba nilisema mimi si Kristo ila nimetumwa nimtangulie. 29 Bibi harusi ni wa bwana harusi. Lakini rafiki yake bwana harusi anayesimama karibu na kusikiliza, hufu rahi aisikiapo sauti ya bwana harusi. Sasa furaha yangu imekamil ika. 30 Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi niwe mdogo zaidi.”

Aliyetoka Mbinguni

31 “Yeye aliyekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote. Anayetoka duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya hapa duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya watu wote. 32 Anayashuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia lakini hakuna anayekubali maneno yake. 33 Lakini ye yote anayekubali maneno yake, anathibitisha kwamba aliyosema Mungu ni kweli. 34 Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu kwa maana Mungu amempa Roho wake pasipo kipimo. 35 Baba anampenda Mwanae na amempa mam laka juu ya vitu vyote. 36 Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica