Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Kgs for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 22:47-71

Yesu Akamatwa

47 Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, pakatokea kundi la watu likiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wana funzi kumi na wawili. Akamsogelea Yesu ili ambusu. 48 Lakini Yesu akamwuliza, “Yuda! Unanisaliti mimi Mwana wa Adamu kwa busu?” 49 Wafuasi wa Yesu walipoona yanayotokea, wakasema, “Bwana, tutumie mapanga yetu?” 50 Na mmoja wao akampiga mtum ishi wa kuhani mkuu kwa panga, akamkata sikio la kulia. 51 Lakini Yesu akasema, “Acheni!” Akaligusa sikio la yule mtu, akamponya. 52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu na wakuu wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mme kuja na mapanga na marungu, kana kwamba mimi ni jambazi? 53 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi lakini hamkunikamata. Lakini wakati huu, ambapo mtawala wa giza anafanya kazi, ndiyo saa yenu.”

Petro Amkana Yesu

54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!” 57 Lakini Petro akakana akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!” 58 Baadaye kidogo mtu mwingine akamwona Petro, akasema, “Wewe pia ni mmoja wao.” Petro akajibu, “Bwana, mimi si mmoja wao!” 59 Baada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akasisitiza, “Kwa hakika huyu mtu alikuwa na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.” 60 Petro akajibu, “Mimi sijui unalosema!” Na wakati huo huo, akiwa bado anazun gumza, jogoo akawika. 61 Yesu akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62 Akaenda nje, akalia kwa uchungu . Yesu Achekwa Na Kupigwa

63 Watu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64 Wakamfunga kitambaa usoni kisha wakasema, “Hebu nabii tuambie! Ni nani amekupiga?” 65 Wakamwambia maneno mengi ya kumtukana. Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza

66 Kulipokucha, Baraza la wazee wa Wayahudi, makuhani wakuu na walimu wa sheria wakakutana. Yesu akaletwa mbele yao. 67 Wakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, tuambie.” Yesu akawa jibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini, 68 na nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 Lakini hivi karibuni, mimi Mwana wa Adamu nita kaa upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.” 70 Wote wakasema, “Ndio kusema wewe ndiye Mwana wa Mungu?” Akawajibu, “Ninyi ndio mmesema kwamba Mimi ndiye.” 71 Kisha wakasema, “Kwa nini tutafute ushahidi zaidi? Sisi wenyewe tumesikia maneno aliy osema.” Yesu Apelekwa Kwa Pilato

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica