Old/New Testament
Kuteketezwa Kwa Yerusalemu
20 “Mkiona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, faham uni kwamba karibu utaangamizwa. 21 Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani; walio mjini Yerusalemu waondoke humo na wale walioko mashambani wasije mjini. 22 Kwa sababu huu utakuwa wakati wa kulipiza kisasi ili yale yote yaliyosemwa kwenye Maan diko yatimie.
23 “Ole wao akina mama watakaokuwa waja wazito na wata kaokuwa wakinyonyesha! Kutakuwa na dhiki nchini na ghadhabu ya Mungu itakuwa juu ya watu wa taifa hili. 24 Wengine watauawa kwa silaha na wengine watachukuliwa mateka na kupelekwa nchi mbalim bali. Na Yerusalemu itamilikiwa na watu wa mataifa mengine mpaka muda wa mataifa hayo utakapokwisha.”
Kuja Kwa Mwana Wa Adamu
25 “Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. 26 Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. 27 Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu. 28 Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.”
29 Akawaambia mfano, “Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Inapochipua majani, mnatambua ya kuwa wakati wa mavuno uko karibu. 31 Hali kadhalika, mkiyaona mambo haya yanatokea, faham uni kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32 Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitakwisha kabla mambo haya hayajatokea. 33 Mbingu na nchi zitatoweka lakini maneno yangu yatadumu daima.” Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafla
34 Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! 35 Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. 36 Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.”
37 Kila siku Yesu alikuwa akifundisha Hekaluni na jioni ili pofika alikwenda kulala kwenye mlima wa Mizeituni. 38 Na asubuhi na mapema watu wote walikuwa wakija Hekaluni kumsikiliza.
Copyright © 1989 by Biblica