Old/New Testament
Yesu Aingia Yerusalemu
28 Alipokwisha kusema haya, Yesu alikaa mbele ya msafara akielekea Yerusalemu. 29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi, 30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa. 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.”’
32 Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana- punda wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?” 34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” 35 Wakamleta kwa Yesu. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, kisha wakampandisha Yesu juu yake. 36 Alipokuwa akienda, watu wakatan daza nguo zao barabarani. 37 Alipokaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote wa wanafunzi wake wakaanza kwa sauti kuu kumsifu Mungu kwa furaha kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona Yesu akifanya, 38 wakasema: “Amebarikiwa Mfalme anayekuja kwa jina la Bwana! Amani mbinguni na Utukufu kwa Mungu.” 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwemo katika umati wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.” 40 Yesu akawajibu, “Nawaambia, hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.”
Yesu Anaulilia Mji Wa Yerusalemu
41 Alipokaribia Yerusalemu, akauona mji, aliulilia,
42 akasema, “Laiti ungalijua leo jinsi ya kupata amani! Lakini sasa huoni! 43 Kuna siku ambapo maadui zako watakuzungushia ukuta na kukuzingira na kukushambulia kutoka kila upande. 44 Watakutupa chini wewe na wanao ndani ya kuta zako na hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine. Hii ni kwa sababu hukutaka kutambua wakati
Yesu Aingia Hekaluni
45 Ndipo akaingia Hekaluni akaanza kuwafukuza wale wal iokuwa wakifanya biashara humo. 46 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala.’ Lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”
47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakiungwa mkono na viongozi wengine walijaribu kila njia wapate kumwua 48 lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote waliomfuata waliyasikiliza maneno yake kwa makini na kuyazingatia. Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake
Copyright © 1989 by Biblica