Old/New Testament
19 1 Yesu akaingia Yeriko, akiwa safarini kuelekea Yerusalemu. 2 Hapo, alikuwapo mtu mmoja mkuu wa watoza kodi na pia mtu tajiri, jina lake Zakayo. 3 Yeye alitamani sana kumwona Yesu lakini hakuweza kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, naye alikuwa mfupi sana. 4 Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu ambaye angepitia njia ile. 5 Yesu alipofika chini ya huo mkuyu, akatazama juu akamwambia: “Zakayo! Shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” 6 Mara moja Zakayo akashuka, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa. 7 Watu wote waliokuwepo, wakaanza kunung’unika, “Amekwenda kuwa mgeni nyumbani kwa mwenye dhambi!” 8 Lakini Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Sikia Bwana, nusu ya mali yangu ninaitoa hivi sasa niwagawie maskini, na kama nimemdhulumu mtu ye yote, nitamrudishia mara nne zaidi.” 9 Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumba hii, kwa sababu huyu naye ni mtoto wa Ibrahimu. 10 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”
Mfano Wa Fedha
11 Wakati walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu aliendelea kuwaambia mfano. Wakati huo watu walikuwa wakidhani kwamba kwa kuwa walikuwa wanakaribia Yerusalemu, Ufalme wa Mungu ungetokea mara. 12 Kwa hiyo akawaambia: “Mtu mmoja wa ukoo wa kitawala, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. 13 Akawaita watumishi wake kumi akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Zitumieni kufanyia biash ara mpaka nitakaporudi.’ 14 Lakini raia wake walimchukia wakapeleka ujumbe usemao, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu. ’ 15 Hata hivyo alipewa ufalme akarudi nyumbani. Kisha akawaita wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu faida kila mmoja wao aliyopata.
16 “Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia nimepata faida mara kumi zaidi.’ 17 Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’
18 “Wa pili naye akaja, akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ 19 Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ 20 Kisha akaja mtumishi mwingine akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’
22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwe nyewe, wewe mtumishi mwovu ! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mkali, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna ambapo sikupanda; 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?’ 24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’ 25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’? 26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho. 27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”’
Copyright © 1989 by Biblica