Old/New Testament
24 Yesu alipoona yule kiongozi amesikitika, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.” 26 Wale waliosi kia hayo wakauliza, “Kama ni hivyo, ni nani basi awezaye kuoko lewa?” 27 Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu yaweze kana kwa Mungu.” 28 Ndipo Petro akasema, “Sisi je? Tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata!” 29 Yesu akajibu, “Nawaam bia hakika, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, ndugu, wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, 30 ambaye hatapewa na Mungu mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika maisha yajayo.” 32 Nitatiwa mikononi mwa watawala wa Kirumi. Watu watanizomea, watanitukana na kunitemea mate. 33 Watanipiga na kuniua, lakini siku ya tatu nitafufuka.”
34 Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya. Maana ya maneno haya ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazun gumzia nini.
Yesu Amponya Kipofu
35 Yesu na wafuasi wake walipokaribia Yeriko, walimpita kipofu mmoja aliyekuwa amekaa kando ya njia, akiomba fedha. 36 Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, “Kuna nini?” 37 Wakamwambia, “Yesu Mnazareti anapita.” 38 Akaita kwa sauti kuu, “Yesu, Mwana wa Daudi! Nionee huruma!” 39 Wale waliokuwa wakiongoza msafara wakamkemea wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi! Nionee huruma!”
40 Yesu akasimama, akaagiza huyo mtu aletwe kwake. Alipo karibia, Yesu akamwuliza, 41 “Unataka nikufanyie nini?” Aka jibu, “Bwana, nataka kuona.”
42 Yesu akamwambia, “Basi upate kuona; imani yako imekupo nya.” 43 Akaweza kuona mara hiyo hiyo akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walioshuhudia mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
Copyright © 1989 by Biblica