Old/New Testament
15 Basi watoza kodi na wenye dhambi wakaja kwa Yesu ili wapate kumsikiliza. 2 Mafarisayo na walimu wa sheria wakaanza kunung’unika, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao!” 3 Ndipo Yesu akawaambia mfano huu: 4 “Tuseme mmoja wenu ana kondoo mia moja halafu mmoja wao apotee. Si ana waacha wale tisini na tisa malishoni aende kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate? 5 Akisha kumpata atambeba mabegani mwake na kwenda nyum bani. 6 Kisha atawaita marafiki na majirani na kuwaambia, ‘Fura hini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’ 7 Nawaam bieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi zake, kuliko ilivyo kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”
Shilingi Iliyopotea
8 “Au tuseme mwanamke ana shilingi kumi halafu apoteze moja. Si atawasha taa afagie nyumba na kutafuta kwa uangalifu mpaka aipate? 9 Na akisha kuipata atawaita marafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile shilingi yangu iliyopotea!’ 10 Vivyo hivyo nawaambia, kuna furaha mbele ya mal aika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi.”
Copyright © 1989 by Biblica