Old/New Testament
Yesu Awaonya Na Kuwafariji Wanafunzi
12 Wakati huo, maelfu ya watu walipokuwa wamekusanyika hata wakawa wanakanyagana, Yesu alizungumza na wanafunzi wake kwanza, akawaambia: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani, unafiki wao.
2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi. 5 Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kumwua mtu ana mamlaka ya kumtupa motoni. Naam: huyo, mwogopeni! 6 Mnajua kwamba mbayuwayu watano huuzwa kwa bei ndogo sana. Lakini Mungu anamjali kila mmoja wao. 7 Mungu anafahamu hata idadi ya nywele zilizoko katika vichwa vyenu. Kwa hiyo msiogope: ninyi mna thamani zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 8 “Ninawaambia, kila atakayenikiri mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkiri mbele ya malaika wa Mungu. 9 Lakini kila anayenikana mbele za watu, pia mimi Mwana wa Adamu nitamkana mbele ya malaika wa Mungu. 10 Na kila atakayesema neno baya kunihusu mimi Mwana wa Adamu atasamehewa. Lakini mtu anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa. 11 “Na watakapowapeleka katika masinagogi mbele ya watawala na mamlaka, msiwe na wasiwasi kuhusu mtakavyojitetea au mtakavyosema: 12 kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”
Mtakatifu atawafundisha mnachopaswa kusema.”
13 Na mtu mmoja katika umati akasema, “Bwana, mwambie ndugu yangu anigawie urithi aliotuachia baba yetu.” 14 Yesu akamwam bia, Rafiki, ni nani aliyenifanya mimi niwe hakimu wenu au mga wanyaji wa urithi wenu?” 15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”
16 Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’ 18 Kisha akasema, ‘Nitafanya hivi: nitabomoa maghala yangu na kujenga maghala makubwa zaidi na huko nitaweka mavuno yangu yote na vitu vyangu. 19 Na nitasema moy oni, ‘Hakika nina bahati! Ninayo mali ya kunitosha kwa miaka mingi. Sasa nitapumzika: nile, ninywe na kustarehe.’ 20 Lakini Mungu akamwambia, ‘Mjinga wewe! Usiku huu huu utakufa! Sasa hivyo vitu ulivyojiwekea vitakuwa vya nani?’ 21 Hivi ndivyo itakavy okuwa kwa mtu ye yote anayehangaika kujikusanyia utajiri duniani lakini si tajiri mbinguni kwa Mungu.”
22 Kisha akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo ninawaambia, msihangaikie maisha yenu, kwamba mtakula nini; au miili yenu kwamba mtavaa nini. 23 Uhai ni zaidi ya chakula; na mwili ni zaidi ya mavazi. 24 Chukueni mfano wa kunguru! Wao hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala po pote pa kuweka nafaka, lakini Mungu anawalisha. Ninyi ni bora zaidi kuliko ndege! 25 Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja? 26 Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo; kwa nini basi mhangaikie hayo mengine? 27 Yata zameni maua yanavyostawi: hayafanyi kazi, wala kujitengenezea nguo; lakini ninawaambia, hata Sulemani katika ufahari wake wote, hakuwahi kuvishwa vizuri kama ua mojawapo! 28 Ikiwa Mungu huyav isha hivi majani ambayo leo yapo shambani na kesho yanachomwa moto; ataachaje kuwavisha ninyi hata zaidi? Mbona mna imani ndogo! 29 Wala msihangaike mtakula nini au mtakunywa nini. Msiwe na wasiwasi juu ya haya. 30 Watu wasiomjua Mungu huhan gaika sana juu ya vitu hivi. Lakini Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnavihitaji. 31 Basi, tafuteni Ufalme wa Mungu; na hivyo vyote atawapatia.”
Copyright © 1989 by Biblica