Old/New Testament
31 Yesu akawau liza, “Niseme nini juu ya watu wa kizazi hiki? Niwafananishe na nini? 32 Wao wamefanana na watoto waliokaa sokoni wakijibizana na wenzao wakisema: ‘Tuliwaimbia nyimbo za shangwe, hamkucheza. Tuliwaimbia nyimbo za msiba, hamkuomboleza.’ 33 Yohana Mbatizaji alikuwa akifunga na hakuonja divai maishani mwake, ninyi mkasema, ‘Ana wazimu!’ 34 Lakini mimi nakula na kunywa, nanyi mnasema: ‘Mtazameni mlafi na mlevi! Rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi.’ 35 Lakini hekima ya Mungu inadhihirishwa kuwa kweli na wote wanaoipokea.”
Mwanamke Aliyempaka Yesu Manukato
36 Farisayo mmoja alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chak ula. Naye akaenda akakaa ale chakula. 37 Katika mji ule palikuwa na mwanamke mmoja kahaba. Naye aliposikia kuwa Yesu atakula nyum bani kwa yule Farisayo, alichukua chupa ya alabasta iliyojaa man ukato 38 akaenda, akakaa nyuma ya Yesu, karibu na miguu yake. Kisha akaanza kulia, machozi yake yakidondokea miguuni mwa Yesu, akayafuta kwa nywele zake. Huku akimbusu miguu na kuimiminia yale manukato.
39 Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Huyu mtu hawezi kuwa ni nabii. Kama ange kuwa nabii angetambua kuwa huyu mwanamke ni kahaba.” 40 Kisha Yesu akijua mawazo ya yule Farisayo akamwambia, “Simoni, kuna jambo nataka kukuambia.” Simoni akajibu “Sema, mwalimu.” 41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: mmoja shillingi elfu tano na mwingine shillingi mia tano. 42 Wote wawili wakashindwa kulipa madeni yao, kwa hiyo akaamua kuwasamehe. Unadhani kati yao, ni yupi aliyempenda zaidi yule aliyewasamehe?” 43 Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesame hewa deni kubwa zaidi.” Yesu akamwambia, “Umejibu sawa.” 44 Ndipo akamgeukia yule mwanamke akamwambia Simoni, “Unamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu, lakini huyu ameniosha miguu kwa machozi yake na kunifuta kwa nywele zake. 45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke amekuwa akiibusu miguu yangu tangu niingie hapa. 46 Hukunipaka mafuta kichwani kama ilivyo desturi lakini huyu mwanamke ameipaka miguu yangu manukato. 47 Kwa hiyo nakuambia, upendo mkubwa aliouonyesha huyu mama unathibitisha kuwa dhambi zake ambazo ni nyingi zimesamehewa. Lakini ye yote asamehewaye kidogo, huonyesha upendo kidogo.”
48 Akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.” 49 Ndipo wale wageni wengine waliokuwepo wakaanza kuulizana, “Hivi huyu ni nani, hata aweze kusamehe dhambi?” 50 Yesu akam wambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”
Copyright © 1989 by Biblica