Old/New Testament
7 Yesu alipomaliza kuwaambia watu mambo haya alikwenda Kaper naumu. 2 Huko mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi ambaye bwana wake alimpenda, alikuwa mgonjwa sana, karibu ya kufa. 3 Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu aliwatuma wazee wa Kiyahudi wakam wombe aje kumponya mtumishi wake. 4 Wale wazee walipofika kwa Yesu walimsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili msaada wako kwani 5 yeye analipenda taifa letu, tena ametujengea sinagogi.”
6 Hivyo Yesu akaongozana nao. Hata alipoikaribia nyumba yake, yule jemadari aliwatuma rafiki zake, kumwambia Yesu, “Bwana, usijisumbue kuingia nyumbani kwangu. Sistahili heshima kubwa kiasi hicho, 7 wala sikuona ninastahili mimi kuja kukuona binafsi. Sema neno moja tu na mtumishi wangu atapona. 8 Katika nafasi yangu ya kazi nina wakubwa wangu na wapo askari wengine chini ya mamlaka yangu. Nikitoa amri kwa askari, ‘Nenda!’ huenda; nikimwambia mwingine, ‘Njoo!’ huja; na nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hiki,’ hufanya.” 9 Yesu aliposikia maneno haya alishangaa sana. Akawageukia wale watu walioongozana naye aka waambia, “Hata katika Israeli yote sijakutana na mtu mwenye imani kama hii.” 10 Na wale waliotumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani kwa yule jemadari walikuta yule mtumishi amepona kabisa.
Yesu Amfufua Mtoto Wa Mjane
11 Baada ya siku hiyo, Yesu alikwenda mji mmoja uitwao Naini. Wanafunzi wake na umati wa watu waliongozana naye. 12 Alipokaribia njia ya kuingia mjini alikutana na watu wal iobeba maiti wakitoka nje ya mji. Marehemu alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa mama mmoja mjane na umati wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mama. 13 Bwana Yesu alipomwona yule mjane moyo wake ulijaa huruma, akamwambia, “Usilie.” 14 Kisha akalisoge lea lile jeneza akaligusa na wale waliolibeba wakasimama. Ndipo akasema: “Kijana nakuambia, amka!” 15 Yule aliyekuwa marehemu akaamka, akakaa na akaanza kusema! Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote wakajawa na hofu. Wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kutuokoa sisi watu wake.” 17 Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi nzima na sehemu za jirani.
Hakuna Aliye Mkuu Kuliko Yohana
18 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walipomweleza Yohana habari hizi zote aliwaita wawili kati yao 19 akawatuma wakamwulize Bwana Yesu, “Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”
21 Wakati huo huo, Yesu aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maumivu na pepo wachafu. Pia akawawezesha vipofu wengi kuona. 22 Ndipo akawajibu wale wanafunzi waliotumwa, “Nendeni mkamwambie Yohana yote mliyoyaona na kusikia: vipofu wanapata kuona, vilema wanatembea, wenye ukoma wanapona, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanasikia Habari Njema. 23 Amebari kiwa mtu asiyepoteza imani yake kwangu.” 24 Wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaeleza watu juu ya Yohana: “Hivi mlipokwenda nyikani mlikwenda kuona nini? Nyasi zikipeperushwa na upepo? 25 Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa nguo za fahari? Sidhani! Watu wanaovaa nguo za fahari na kuishi maisha ya anasa hukaa katika majumba makubwa. 26 Sasa mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kuona nabii? Naam! Tena aliye mkuu kuliko nabii. 27 Huyu Yohana ndiye anayezungumzwa katika Maandiko yase mayo: ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie, ili akuandalie njia.’ 28 Nawaambia, kati ya binadamu wote, hakuna aliye mkuu kumzidi Yohana. Hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. 29 Watu wote waliosikia maneno hayo, ikiwa ni pamoja na watoza ushuru, walimtukuza Mungu kwa kuwa wao waliukubali ubatizo wa Yohana. 30 Bali Mafarisayo na wanasheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokukubali kubatizwa na Yohana.
Copyright © 1989 by Biblica