Old/New Testament
Yesu Amponya Mwenye Kupooza
17 Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na wal imu wa sheria kutoka katika kila mji wa wilaya za Galilaya, Yudea na Yerusalemu walikuwepo. Na Yesu alikuwa amejaa nguvu ya Mungu ya kuponya wagonjwa.
18-19 Kisha wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwe nye kitanda. Wakajaribu kumpitisha ndani wamfikishe alipokuwa Yesu, lakini wakashindwa kwa sababu ya msongamano wa watu. Basi wakampandisha juu ya paa, wakaondoa baadhi ya vigae, wakapata nafasi ya kumteremsha yule mgonjwa pamoja na kitanda chake kwa kamba, hadi mbele ya Yesu. 20 Alipoona imani yao, Yesu alimwam bia yule mgonjwa, “Rafiki yangu, umesamehewa dhambi zako.” 21 Wale walimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kusemezana, “Mbona huyu anakufuru! Anadhani yeye ni nani? Hakuna awezae kusamehe dhambi ila Mungu peke yake.”
22 Yesu alifahamu mawazo yao kwa hiyo akawauliza, “Kwa nini mnafikiri mimi ninakufuru? 23 Je, ni lipi lililo rahisi zaidi, kumwambia huyu, ‘Umesamehewa dhambi zako’; au kusema, ‘Simama utembee?’ 24 Sasa nitawahakikishia kuwa mimi Mwana wa Adamu ninao uwezo wa kusamehe dhambi duniani.” Akamgeukia yule mgonjwa aliyepooza, akasema, “Nakuambia: Simama! Chukua kitanda chako uende nyumbani.” 25 Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu. 26 Wote waliokuwepo wakastaajabu sana. Wakajaa hofu. Wakamtukuza Mungu, wakasema, “Tumeona maajabu leo.”
Yesu Amwita Lawi
27 Baada ya haya Yesu alimwona afisa mmoja mtoza kodi jina lake Lawi akiwa ofisini mwake, akamwambia, “Njoo uwe mmoja wa wanafunzi wangu.” 28 Lawi akaacha vyote, akaondoka, akamfuata Yesu. 29 Baadaye Lawi akafanya karamu kubwa kumkaribisha Yesu nyumbani kwake. Watoza kodi wengi walikuwa miongoni mwa watu wal ioalikwa. 30 Basi baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria ambao walikuwa kundi moja wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu wakisema, “Mbona mnakula na kunywa na wenye dhambi?” 31 Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 32 Sikuja kwa ajili ya wenye haki bali nimekuja kuwaita wenye dhambi ili watubu.”
Yesu Aulizwa Habari Za Kufunga
33 Baadhi ya watu wakamwuliza Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na kusali mara kwa mara. Mbona wanafunzi wako wanakula na kunywa tu?”
34 Yesu akawajibu, “Je, inawezekana wageni walioalikwa har usini kufunga wakati wakiwa na Bwana Harusi? 35 Lakini wakati utafika ambapo Bwana Harusi ataondolewa. Wakati huo ndipo wataka pofunga.
36 Yesu akawapa mfano akawaambia: “Hakuna mtu anayechana nguo mpya ili apate kiraka cha kuweka kwenye nguo kuu kuu. Akifa nya hivyo ataharibu ile nguo mpya na ile kuu kuu itaonekana mbaya zaidi ikiwa na kiraka kipya. 37 Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vilivyochakaa; ukifanya hivyo, hivyo viriba vitapa suka na divai yote itamwagika. 38 Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 39 Na pia hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai iliyoiva vizuri. Kwa maana husema, ‘Hii divai iliyoiva siku nyingi ni bora zaidi.’ ”
Copyright © 1989 by Biblica