Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Josh for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 1:21-38

21 Wakati mambo haya yakitokea mle Hekaluni, watu waliokuwa nje wakimngojea Zakaria walikuwa wakishangaa kwa nini alikawia kutoka. 22 Hati maye alipotoka hakuweza kusema nao. Wakatambua ya kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Kwa kuwa alikuwa bubu, akawaashiria kwa mikono. 23 Muda wake wa zamu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. 24 Kisha baada ya muda si mrefu, Elizabeti mkewe alipata mimba, naye akajificha kwa miezi mitano akisema: 25 “Bwana amekuwa mwema kwangu. Maana ameniondolea aibu yangu mbele za watu.”

Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa

26 Miezi sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alim tuma malaika Gabrieli aende katika mji wa Nazareti, ulioko Gali laya, 27 kwa msichana bikira aliyeitwa Mariamu. Yeye alikuwa ameposwa na mtu mmoja aliyeitwa Yusufu, wa ukoo wa Mfalme Daudi.

28 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Sal aamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”

29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini. 30 Ndipo malaika akamwam bia, “Usiogope, Mariamu, Mungu amependezwa nawe. 31 Sikiliza, utapata mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; na utamwita jina lake Yesu. 32 Mtoto huyo atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Mfalme Daudi, baba yake. 33 Atatawala juu ya nyumba ya Yakobo daima; na ufalme wake hau takuwa na mwisho!”

34 Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba, na mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu ata kujilia na nguvu za Mungu zitakufunika kama kivuli, na kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu na ataitwa Mwana wa Mungu. 36 Tena, miezi sita iliyopita binamu yako Elizabeti, aliyeitwa tasa, amepata mimba ingawa ni mzee sana. 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”

38 Mariamu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.’ ’ Kisha malaika akaondoka.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica