Old/New Testament
Amri Iliyo Kuu
28 Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” 29 Yesu akamjibu, “Iliyo kuu ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee. 30 Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ 31 Na sheria ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
32 Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, ume jibu vyema. Ulivyosema ni kweli kabisa, Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Na kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote; na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa.”
34 Yesu alipoona jinsi alivyojibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali zaidi.
Kuhusu Mwana Wa Daudi
35 Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, “Mbona walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? 36 Kwa maana Daudi akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: keti mkono wangu wa kulia mpaka niwashi nde na kuwafedhehesha maadui zako chini ya miguu yako.’ 37 Ikiwa Daudi mwenyewe anamwita Bwana, yawezekanaje tena Kristo akawa mwanawe?” Watu wote wakamsikiliza kwa furaha.
Yesu Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Shera
38 Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yao rasmi na kusalimiwa kwa heshima masokoni. 39 Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za heshi ma katika sherehe. 40 Hao hao ndio huwadhulumu wajane nyumba zao na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Mungu ata waadhibu vikali zaidi.”
Sadaka Ya Mjane
41 Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. 42 Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
43 Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! 44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”
Copyright © 1989 by Biblica