Old/New Testament
Yesu Aingia Yerusalemu
11 Walipokaribia Yerusalemu, wakiwa katika miji ya Bethfage na Bethania katika mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili watangulie. 2 Akawaagiza, “Nendeni kwenye kijiji kile kilichoko mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtam wona mwana punda amefungwa, ambaye hajawahi kupandwa na mtu ye yote. Mfungueni mumlete hapa. 3 Kama mtu atawauliza, ‘Mbona mnam fungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji na atamrudisha mara moja.’ ” 4-5 Wakaenda, wakamkuta mwana punda mmoja kando ya barabara, akiwa amefungwa kwenye mlango wa nyumba. Walipokuwa wakimfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwanapunda?” 6 Wakawajibu kama Yesu alivyokuwa amewaagiza, na wale watu wakawaruhusu.
7 Wakamleta huyo mwana punda kwa Yesu wakamtandikia mavazi yao, akaketi juu yake. 8-10 Watu wengi wakatandaza nguo zao barabarani na wengine wakatandaza matawi waliyokata mashambani. Na wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti zao wakasema: “Hosana! Mungu apewe sifa! Mungu ambariki yeye anayekuja kwa jina la Bwana! Ubarikiwe Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Mungu asifiwe!”
11 Yesu akaingia Yerusalemu, akaenda Hekaluni akaangalia kila kitu. Lakini kwa kuwa ilikuwa jioni, akaenda Bethania na wale wanafunzi kumi na wawili.
Yesu Alaani Mtini Usiozaa
12 Kesho yake walipokuwa wanaondoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. 13 Alipouona mtini kwa mbali, alikwenda kuangalia kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, alikuta una majani tu kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 14 Yesu akauambia ule mti, “Hakuna mtu atakayekula tini kutoka kwako tena.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Yesu Afukuza Wafanya Biashara Hekaluni
15 Walipofika Yerusalemu, Yesu aliingia Hekaluni akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakifanya biashara humo. Akapindua meza za waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya watu waliokuwa wakiuza njiwa. 16 Hakuruhusu mtu ye yote kuchukua bidhaa kupi tia ukumbi wa Hekalu. 17 Akawafundisha akisema, “Je, haikuan dikwa katika Maandiko kuwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa watu wote’? Mbona ninyi mmeigeuza kuwa pango la wany ang’anyi?”
18 Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakapata habari. Wakatafuta njia ya kumwangamiza. Walimwogopa kwa sababu watu wal ikuwa wamevutiwa sana na mafundisho yake.
Copyright © 1989 by Biblica