Old/New Testament
9 Yesu akaendelea kuwaambia, ‘ ‘Ninawahakikishia kuwa wapo watu hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”
Yesu Ageuka Sura
2 Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana akawapeleka juu ya mlima mrefu ambapo walikuwa faraghani, peke yao. Na huko, wakiwa wanamtazama, Yesu akageuka sura. 3 Mavazi yake yakametameta kwa weupe, yakang’aa, yakawa meupe kuliko ambavyo dobi ye yote duniani angaliweza kuyang’aarisha. 4 Musa na Eliya wakawatokea nao walikuwa wakizungumza na Yesu.
5 Petro akamwambia Yesu , “Mwalimu, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Tutengeneze vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Musa na kingine cha Eliya.” 6 Petro hakujua aseme nini kwa maana yeye na wenzake walikuwa wameogopa sana.
7 Ndipo pakatokea wingu, likawafunika, na sauti kutoka katika wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu nimpendaye, msikilizeni yeye.” 8 Mara walipotazama huku na huku hawakuona mtu mwingine tena isipokuwa Yesu.
9 Walipokuwa wakiteremka mlimani, Yesu akawakataza wasim wambie mtu ye yote mambo waliyoona, mpaka yeye Mwana wa Mungu atakapofufuka kutoka kwa wafu. 10 Wakatii agizo hilo, lakini wakawa wanajadiliana kati yao maana ya ‘Kufufuka kutoka kwa wafu.’ 11 Wakamwuliza, “Kwa nini walimu wa sheria husema kwamba ni lazima Eliya aje kwanza kabla mambo haya hayajatokea?’ ’ 12 Yesu akawajibu, “Ni kweli, Eliya anakuja kwanza kusawazisha mambo yote. Hata hivyo, mbona imeandikwa kwamba Mimi, Mwana wa Adamu ni lazima niteseke sana na kudharauliwa? 13 Lakini nina waambia, Eliya amekwisha kuja na wamemtendea walivyopenda, kama Maandiko yasemavyo juu yake.”
Yesu Amponya Mvulana Mwenye Pepo
14 Walipowafikia wale wanafunzi wengine, waliwakuta wame zungukwa na umati mkubwa wa watu na baadhi ya walimu wa sheria wakibishana nao. 15 Mara wale watu walipomwona Yesu, walistaaj abu sana, wakamkimbilia, wakamsalimu. 16 Akawauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nini nao?”
17 Mtu mmoja katika ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nimemleta kwako mtoto wangu wa kiume kwa maana amepagawa na pepo ambaye amemfanya kuwa bubu. 18 Kila mara pepo huyo amwingiapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Nimewaomba wanafunzi wako wamtoe pepo huyo, lakini hawakuweza.”
19 Yesu akawaambia, “Ninyi kizazi kisicho na imani! Nita kuwa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni huyo mtoto kwangu!” 20 Wakamleta. Yule pepo alipomwona Yesu, alimtia yule mvulana kifafa, akaanguka chini akajiviringisha viringisha huku akitokwa na povu mdomoni. 21 Yesu akamwuliza baba yake, “Mwanao amekuwa na hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake. 22 Na mara nyingi huyo pepo amemwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kuangamiza maisha yake. Lakini kama wewe unaweza kufanya cho chote, tafadhali tuonee huruma, utusaidie.” 23 Yesu akasema, “Kama unaweza! Kila kitu kinawezekana kwa mtu mwenye imani.” 24 Ndipo yule baba akasema kwa sauti, “Ninaamini. Nisaidie niweze kuamini zaidi!” 25 Naye Yesu ali poona umati wa watu unazidi kusongana kuja hapo walipokuwa, akam kemea yule pepo mchafu akisema, “Wewe pepo bubu na kiziwi, naku amuru umtoke, usimwingie tena!” 26 Yule pepo akapiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu kisha akatoka. Yule mvulana alionekana kama amekufa; kwa hiyo watu wengi wakasema, “Amekufa.” 27 Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua, naye akasimama.
28 Walipokwisha kuingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza wakiwa peke yao, “Mbona sisi hatukuweza kumtoa huyo pepo?” 29 Yesu akawajibu, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isi pokuwa kwa maombi.”
Copyright © 1989 by Biblica