Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Num for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Marko 7:14-37

14 Yesu akaita tena ule umati wa watu akawaambia, “Nisiki lizeni nyote kwa makini na muelewe. 15 Hakuna kitu kinachomwin gia mtu kutoka nje ambacho kinaweza kumfanya mchafu. Kitu kina chotoka ndani yake ndicho kinachomfanya mchafu. 16 Mwenye nia ya kusikia na asikie.”

17 Alipoachana na wale watu aliingia ndani. Wanafunzi wake wakamwuliza maana ya mfano ule. 18 Akawajibu, “Hata nanyi hamwelewi? Hamtambui kwamba kitu kimwingiacho mtu kutoka nje hakiwezi kumfanya mchafu? 19 Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje. Kwa kusema hivi, Yesu alifundisha kuwa aina zote za vyakula ni halali kuliwa.

20 Akaendelea kusema, “Kile kitokacho ndani ya mtu ndicho kinachomfanya awe mchafu. 21 Kwa maana ndani ya mtu, yaani moy oni mwake, hutoka: mawazo mabaya, uasherati, 22 wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matusi, kiburi na upumbavu. 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, na ndio yanayomfanya mchafu.”

Yesu Amponya Binti Ya Mama Mtaifa

24 Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia nyumba moja, ambapo hakupenda mtu afahamu yupo. Lakini hakuweza kujificha. 25 Mama mmoja ambaye binti yake mdogo ali kuwa na pepo mchafu aliposikia habari za Yesu, alikuja mara moja akajiangusha miguuni pake. 26 Huyo mama hakuwa Myahudi, alikuwa Mgiriki aliyezaliwa Siria-Foinike. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.

27 Yesu akamwambia, “Tuwaache watoto wale washibe kwanza, kwa maana si halali kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

28 Yule mama akajibu, “Ni kweli Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.” 29 Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, unaweza kwenda nyumbani. Yule pepo ameshamtoka binti yako.”

30 Akaenda nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo amemtoka.

Yesu Amponya Mtu Aliyekuwa Bubu Na Kiziwi

31 Yesu akaondoka katika eneo la Tiro, akapita katikati ya Sidoni akaenda hadi Ziwa la Galilaya kwa kupitia katika eneo la Dekapoli. 32 Hapo, watu walimletea kiziwi mmoja ambaye pia alikuwa hawezi kusema sawa sawa, wakamwomba amwekee mikono ili apone. 33 Yesu akampeleka yule kiziwi kando mbali na watu, akain giza vidole masikioni mwake kisha akatema mate na akaugusa ulimi wake. 34 Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akahema kwa uchungu, akamwambia, “Efatha!” yaani “Funguka!” 35 Wakati huo huo masikio ya yule mtu yakafunguka na ulimi wake ukawa huru akaanza kusema vizuri.

36 Yesu akawaamuru wasimwambie mtu ye yote habari hizi. Lakini kadiri alivyowazuia ndivyo walivyozidi kutangaza habari zake. 37 Watu wakastaajabu mno. Wakasema, “Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica