Old/New Testament
Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda mahali pasipo na watu.
33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda. Wakawahi kufika.
34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda. 36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba na vijiji vya jirani.”
37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya kutosha kulisha watu wote hawa.”
38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”
39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.
Yesu Atembea Juu Ya Maji
45 Wakati huo huo Yesu akawaamuru wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye anawaaga watu. 46 Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kusali. 47 Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imeshafika katikati ya ziwa na Yesu alikuwa peke yake nchi kavu. 48 Aliwaona wanafunzi wake wakihangaika na kuvuta makasia kwa nguvu kwa sababu upepo ulikuwa ukielekea walikotoka. Karibu na mapambazuko, Yesu aka waendea wanafunzi wake akitembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, walid hani ni mzimu, wakapiga yowe, 50 kwa maana wote walimwona wakaogopa. Lakini mara Yesu akasema nao, “Tulieni! Ni mimi, msi ogope!” 51 Akapanda kwenye mashua yao na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa. 52 Walikuwa bado hawajaelewa hata maana ya u le muujiza wa mikate. Walikuwa bado hawajafunuliwa akilini mwao.
53 Walipokwisha kuvuka, walifika katika wilaya ya Gene zareti, wakatia nanga. 54 Waliposhuka kutoka katika mashua yao, watu walimtambua Yesu mara moja, 55 wakapita vijiji vyote haraka haraka, wakawabeba wagonjwa kwenye machela wakamfuata mahali po pote waliposikia kuwa yupo. 56 Na kila mahali Yesu alipokwenda, ikiwa ni vijijini, mijini na mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa angalao waguse pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.
Copyright © 1989 by Biblica