Old/New Testament
Mfano Wa Taa
21 Akawaambia tena, “Je, mtu anapowasha taa, huifunika kwa bakuli au kuiweka mvunguni? Si anaiweka mahali pa wazi? 22 Hali kadhalika, kila kilichofichwa kitatolewa hadharani; na kila siri itafichuliwa. 23 Mwenye nia ya kusikia, na asikie.”
24 Akaendelea kuwaambia, “Myaweke maanani haya mnayosikia. Kipimo mnachotumia kwa wengine ndicho kitakachotumiwa kuwapima na ninyi, hata na zaidi. 25 Kwa maana aliye na kitu ataongezewa, na asiye na kitu atanyang’anywa hata kile kidogo alicho nacho.”
Mfano Wa Jinsi Mbegu Inavyoota
26 Akawaambia tena, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 27 Akishazipanda, usiku hulala na mchana huamka, wakati huo mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua inakuaje. 28 Udongo wenyewe huwezesha mimea hiyo kuchipua, kukua na kukomaa. 29 Mavuno yanapokuwa tayari, bila kupoteza wakati, yule mkulima huleta mtu akaikata hiyo mimea kwa kuwa wakati wa kuvuna umefika.”
Mfano Wa Mbegu Ya Haradali
30 Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuuelezea? 31 Tunaweza kuufa nanisha na punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. 32 Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wakaweza kujenga viota kwenye kiv uli chake.”
33 Yesu alitumia mifano mingine mingi kama hii kuwaelezea neno la Mungu, kwa kadiri walivyoweza kuelewa. 34 Hakuwafundisha lo lote kuhusu Ufalme wa Mungu pasipo kutumia mifano. Lakini ali pokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.
Yesu Atuliza Dhoruba
35 Siku hiyo, ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke, twende ng’ambo ya pili.” 36 Wakawaacha wale watu wakaingia katika ile mashua ambamo Yesu alikuwa amekaa. Pia palikuwa na mashua nyingine.
37 Pakatokea dhoruba kali, mawimbi yakaipiga ile mashua waliyokuwa wakivukia, ikaanza kujaa maji. Yesu alikuwa amelala akiegemea mto sehemu ya nyuma kwenye ile mashua. 38 Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kwamba tuna zama?’ 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akaiambia ile bahari, “Kaa kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari.
40 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa? Je, bado hamna imani?”
41 Lakini wao walikuwa wamejawa na hofu wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”
Copyright © 1989 by Biblica