Old/New Testament
Yesu Na Beelzebuli
20 Yesu akarudi nyumbani. Umati wa watu ukamfuata tena, hata yeye na wanafunzi wake wakashindwa kula chakula. 21 Ndugu zake walipopata habari walikuja kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”
22 Walimu wa sheria waliotoka Yerusalemu walikuwa wakisema, “Amepagawa na Beelzebuli, mkuu wa mashetani; na ni kwa uwezo wa Beelzebuli anawafukuza mashetani.”
Beelzebuli anawafukuza mashetani.”
23 Basi Yesu akawaita akazungumza nao kwa mifano: “Shetani awezaje kufukuza shetani? 24 Ikiwa utawala wa nchi umegawanyika wenyewe, hauwezi kudumu. 25 Hali kadhalika kama jamaa moja ime gawanyika yenyewe kwa yenyewe, jamaa hiyo haiwezi kudumu. 26 Na kama shetani akijipiga vita yeye mwenyewe hatatimiza cho chote ila mwisho wake umekaribia. 27 Pia hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumwibia vitu vyake vyote pasipo kwanza kumfunga huyo mwenye nyumba mwenye nguvu. Akisha mfunga, ndipo anaweza kumwibia kila kitu.
28 “Nawaambieni kweli, dhambi zote watendazo wanadamu na maneno yote ya kufuru wasemayo, watasamehewa. 29 Lakini ye yote anayemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” 30 Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema ana pepo mchafu.
Mama Na Ndugu Wa Yesu
31 Mama yake Yesu na ndugu zake wakafika wakasimama nje wakamtuma mtu amwite. 32 Umati wa watu waliokuwa wameketi kum zunguka wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wana kutafuta.”
33 Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?”
34 Akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka, akasema, “Hawa ndio mama zangu na ndugu zangu. 35 Mtu ye yote anayetenda mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.”
Copyright © 1989 by Biblica