Old/New Testament
23 Wakati huo huo, mtu mmoja aliyekuwa na pepo 24 akapiga kelele humo katika sinagogi akasema, “Mbona unatuingilia, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninafahamu wewe ni nani! Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 25 Lakini Yesu akamkemea akamwambia, “Kaa kimya! Mtoke!” 26 Yule pepo mchafu akamtikisa yule mtu kwa nguvu kisha akamtoka akipiga kelele.
27 Watu wakashangaa, wakaanza kuulizana, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya? Huyu mtu anatoa amri kwa mamlaka na hata pepo wanamtii!”
28 Sifa zake zikaenea upesi kila mahali katika mkoa wote wa
Yesu Amponya Mama Mkwe Wa Simoni
29 Yesu na wanafunzi wake walipoondoka katika sinagogi, walikwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. Wanafunzi wengine waliokuwepo ni Yakobo na Yohana. 30 Mama mkwe wake Simoni alikuwa kitandani, ana homa. Na mara Yesu alipofika wakamweleza. 31 Yesu akaenda karibu na kitanda, akamshika yule mama mkono, akamwinua; homa ikamtoka, akawahudumia.
Yesu Aponya Wengi
32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni nani.
Yesu Aondoka Kapernaumu Na Kwenda Galilaya
35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda mahali pa faragha, akaomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta. 37 Walipomwona wakamwambia, “Kila mtu ana kutafuta!”
38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.” 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya nzima akihubiri katika masinagogi na kuponya watu waliopagawa na pepo.
Yesu Amponya Mtu Mwenye Ukoma
40 Akaja mtu mwenye ukoma, akapiga magoti mbele ya Yesu akamsihi, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.” 41 Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka upone, takasika.” 42 Mara ukoma wote ukaisha akapona kabisa. 43 Yesu akamruhusu aende lakini 44 akamwonya, “Usimwambie mtu ye yote habari hizi; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka ya utakaso kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwa watu.”
45 Lakini yule mtu alikwenda akatangaza habari za kuponywa kwake kila mahali. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia katika vijiji na miji waziwazi isipokuwa alikaa sehemu zisizo na watu, nao wakamfuata huko kutoka pande zote.
Copyright © 1989 by Biblica