Old/New Testament
Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji
1 Huu ni mwanzo wa Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2 Kama alivyoandika nabii Isaya, Mungu alisema: “Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye ataandaa njia yako.” 3 “Mtu aitaye kwa sauti kuu jangwani. ‘Mtengenezeeni Bwana njia; nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”
4 Yohana alitokea nyikani, akawabatiza watu huko na kuwahubi ria kwamba watubu, wabatizwe, ili wasamehewe dhambi zao. 5 Watu kutoka eneo lote la Yudea na sehemu zote za Yerusalemu walikwenda kumsikiliza. Wakatubu dhambi zao, akawabatiza katika mto wa Yor dani. 6 Yohana alivaa mavazi ya manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa ni nzige na asali ya mwituni. 7 Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye uwezo kunizidi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. 8 Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawaba tiza kwa Roho Mtakatifu.”
Yesu Abatizwa
9 Baadaye Yesu akaja kutoka Nazareti katika sehemu ya Gali laya, akabatizwa na Yohana katika mto wa Yordani. 10 Yesu alipo toka kwenye maji aliona mbingu zikifunuka na Roho wa Mungu anam shukia kama njiwa. 11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa; nimependezwa nawe.”
Yesu Ajaribiwa Nyikani
12 Mara tu baada ya haya, Roho akamwongoza Yesu mpaka nyikani. 13 Akakaa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini aki jaribiwa na shetani. Alikaa na wanyama wa porini na malaika wal imhudumia.
Yesu Aanza Kuhubiri
14 Yohana mbatizaji alipokamatwa na kutiwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya akaanza kutangaza Habari Njema za Mungu, 15 akisema, “Wakati umefika: Ufalme wa Mungu umewasili. Tubuni, muamini Habari Njema.”
Yesu Awaita Wanafunzi Wanne
16 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa la Galilaya alimwona Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa kutumia nyavu; ndugu hawa wawili walikuwa wavuvi. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” 18 Wakaacha nyavu zao mara moja wakamfuata Yesu.
19 Alipokwenda mbele kidogo, akawaona Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo. Wao walikuwa katika mashua wakitengeneza nyavu zao. 20 Mara tu alipowaona akawaita, nao wakamwacha baba yao na wavuvi wa kuajiriwa, wakamfuata Yesu.
Yesu Afukuza Pepo Mchafu
21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda katika sinagogi akaanza kufundisha. 22 Watu waliom sikiliza, walishangazwa sana na mafundisho yake. Yeye hakufund isha kama walimu wao wa sheria. Alifundisha kama mtu mwenye mam laka.
Copyright © 1989 by Biblica