Old/New Testament
51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52 Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliofariki ili fufuka. 53 Walitoka makaburini na Yesu alipofufuka walikwenda Mji Mtakatifu wakawatokea watu wengi. 54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yote yaliyotokea, waliogopa wakasema, “Hakika, huyu alikuwa
Mwana wa Mungu!”
55 Wanawake wengi walio kuwa wamefuatana na Yesu tangu Gali laya wakimhudumia, nao walikuwapo wakitazama kwa mbali yote yali yotokea. 56 Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo na Yusufu na mama yao wana wa Zebedayo.
Yesu Azikwa Kaburini
57 Ilipofika jioni, alifika tajiri mmoja kutoka Arimathea aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akaenda kwa Pilato akaomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59-60 Yusufu alichukua mwili wa Yesu akauweka katika sanda safi akauzika katika kaburi lake jipya ambalo lilikuwa limechongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe kubwa akafu nika mlango wa kaburi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikuwa wamekaa mbele ya kaburi.
Walinzi Wa Kaburi
62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.” 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka askari walinzi.
Copyright © 1989 by Biblica