Old/New Testament
Askari Wamdhihaki Yesu
27 Kisha askari wa gavana wakampeleka Yesu kwenye makao makuu ya gavana wakakusanya kikosi cha askari, wakamzunguka Yesu.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu ya rangi nyekundu. 29 Wakasokota taji ya miiba wakamvika kichwani. Wakamwekea fimbo mkono wake wa kulia, wakapiga magoti mbele zake wakamdhihaki wakisema, “Uishi maisha marefu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga nayo kich wani. 31 Baada ya kumdhihaki, walimvua ile kanzu, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka kumsulubisha.
Yesu Asulubishwa
32 Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakambebesha ule msalaba kwa nguvu. 33 Na wali pofika sehemu iitwayo Golgotha, maana yake mahali pa Fuvu la Kichwa, 34 wakampa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini baada ya kuionja, akaikataa.
35 Walipokwisha kumsulubisha wakagawana nguo zake kwa kuzi pigia kura. 36 Kisha wakaketi, wakamchunga. 37 Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.’ 38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja kulia kwake na mwingine kushoto kwake.
39 Watu waliokuwa wakipita njiani walimtukana, wakatikisa vichwa vyao 40 na kusema, “Si ulisema ungevunja Hekalu na kulijenga kwa muda wa siku tatu? Jiokoe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu shuka msalabani.” 41 Hali kadhalika, makuhani wakuu, walimu wa sheria na wazee walimdhihaki, wakisema, 42 “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye si Mfalme wa Israeli? Ashuke kutoka msalabani nasi tutamwamini. 43 Anamwamini Mungu; basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka. Kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 44 Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa naye walimtukana kwa njia hiyo hiyo.
Kifo Cha Yesu
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?”
47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu].
50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho.
Copyright © 1989 by Biblica