Old/New Testament
Yesu Apelekwa Kwa Pilato
27 Asubuhi na mapema, makuhani wakuu wote na wazee walifanya mkutano, wakashauriana jinsi ya kumwua. 2 Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato ambaye alikuwa gavana.
Majuto Ya Yuda
3 Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehuku miwa alijuta. Akazirudisha zile fedha alizopewa kwa makuhani wakuu na wazee 4 akawaambia, “Nimetenda dhambi kwa maana nimem saliti mtu asiye na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”
5 Basi Yuda akazitupa zile fedha Hekaluni, akaondoka; akaenda akajinyonga.
6 Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” 7 Kwa hiyo baada ya kujadiliana waliamua kuzitumia kununua shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. 8 Kwa hiyo shamba hili limeitwa ‘Shamba la damu’ hadi leo. 9 Ndipo yakatimia yale aliyonena nabii Yeremia kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na wana wa Israeli, 10 wakanunulia shamba la mfinyanzi kama Bwana alivyon iagiza.”
Yesu Mbele Ya Pilato
11 Yesu akapelekwa mbele ya gavana naye akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Hayo umetamka wewe.” 12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipomshtaki kwa mambo mengi hakujibu neno. 13 Ndipo Pilato akamwuliza, “Husikii mambo hayo yote wanayokushtaki nayo?” 14 Lakini Yesu hakujibu neno hata kwa shtaka moja. Gavana akashangaa sana.
15 Kila wakati wa sikukuu, gavana alikuwa na desturi ya kum fungua mfungwa mmoja atakayechaguliwa na watu. 16 Wakati huo alikuwapo mfungwa mmoja mwenye kujulikana sana, aliyeitwa Baraba. 17 Basi watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwa fungulie nani; Baraba au Yesu aitwaye Kristo?” 18 Kwa sababu alijua kuwa Yesu aliletwa kwake kwa ajili ya wivu wa viongozi wa Wayahudi. 19 Alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mke wake alimpelekea ujumbe, “Usijihusishe katika kesi ya huyu mtu asiye na hatia. Leo nimehangaika sana katika ndoto kwa ajili yake.”
20 Basi makuhani na wazee wakawashawishi umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe. 21 Gavana akawau liza tena , “Ni yupi mnataka niwafungulie?” Wakajibu, “Bar aba!” 22 “Sasa nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote , “Asulubiwe!” 23 Akasema, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Asulubiwe.”
24 Pilato alipoona kwamba hakuna zaidi ambalo angeweza kufa nya na kwamba ghasia ilikuwa ikianza, akachukua maji, akanawa mikono mbele yao, akasema, “Sina hatia na damu ya mtu huyu. Jambo hili ni juu yenu.”
Jambo hili ni juu yenu.”
25 Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”
26 Basi akawafungulia Baraba, na baada ya kuamuru Yesu apigwe viboko, akamtoa asulubiwe.
Copyright © 1989 by Biblica