Old/New Testament
51 Ndipo mmojawapo wa wafuasi wa Yesu ali poona hivyo, akachukua panga lake, akampiga nalo mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 52 Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. 53 Unadhani siwezi kumwomba Baba yangu aniletee mara moja majeshi kumi na mbili ya malaika? 54 Lakini nikifanya hivyo yatatimiaje Maandiko yale yasemayo kwamba mambo haya lazima yato kee?”
55 Wakati huo Yesu akawaambia ule umati, “Mmekuja kunika mata kama mnyang’anyi kwa mapanga na marungu? Mbona siku zote nilikaa Hekaluni na kufundisha lakini hamkunikamata? 56 Lakini haya yametokea ili Maandiko ya manabii yatiimie.” Ndipo wana funzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.
Yesu Ashtakiwa Mbele Ya Baraza
57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekutanika.
58 Lakini Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu akaingia ndani pamoja na walinzi aone litakalotokea. 59 Basi makuhani wakuu na baraza zima wakatafuta ushahidi wa uongo ili wamwue Yesu, 60 lakini hawakupata, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza watu wawili, 61 wakasema: “Huyu mtu alisema, ‘Nina uwezo wa kuvunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena katika muda wa siku tatu .’ ”
62 Kisha kuhani mkuu akasimama, akamwambia Yesu, “Huna jibu? Husikii huo ushahidi waliotoa watu hao?” 63 Lakini Yesu hakusema neno. Basi kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa jina la Mungu aliye hai, tuambie kama wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.”
Mungu.”
64 Yesu akajibu, “Umetamka mwenyewe. Lakini nina waambieni nyote kwamba baada ya hapa, mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa Mungu mwenye uweza na akija juu ya mawingu ya mbin guni.”
65 Aliposikia maneno hayo, kuhani mkuu alirarua mavazi yake akasema, “Amekufuru! Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Si mmemsi kia akikufuru? 66 Mnaamuaje?” Wakajibu, “Anastahili kufa!”
67 Kisha wakamtemea mate usoni; wengine wakampiga ngumi na makofi, 68 wakasema, “Hebu toa unabii wewe Kristo! Ni nani ame kupiga?”
69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui usemalo.”
71 Kisha alipotoka nje, mlangoni mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwapo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Simfa hamu mtu huyo!” 73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesi mama pale walimwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao kwa maana namna yako ya kusema ni kama yao.” 74 Ndipo Petro akalaani na kuapa, akawaambia, “Simfahamu mtu huyo!” Wakati huo huo jogoo akawika. 75 Na Petro akakumbuka Yesu alivyomwambia, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.” Akaenda nje, akalia kwa uchungu.
Copyright © 1989 by Biblica