Old/New Testament
29 “Mara baada ya dhiki ya wakati huo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake tena, na nyota zitaanguka kutoka mbin guni; nguvu za anga zitatikisika. 30 Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu angani na watu wote ulimwenguni wataomboleza. Nao wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. 31 Na nitawatuma malaika zangu kwa sauti kuu ya tarumbeta na watawakusanya wateule wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.
32 “Jifunzeni kutoka kwa mti wa mtini. Matawi yake yana poanza kuwa laini na majani kuchipua, mnafahamu kwamba kiangazi kimekaribia. 33 Basi, pia mkiona dalili hizi, fahamuni kwamba amekaribia kurudi, na yu karibu na mlango. 34 Nawaambieni kweli, hakika kizazi hiki hakitapita kabla mambo haya hayajatokea. 35 Mbingu na dunia zitatoweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa
36 “Hakuna ajuaye siku wala saa, hata malaika mbinguni wala Mwana, isipokuwa Baba peke yake. 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.
40 “Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa. 41 Wanawake wawili watakuwa wanatwanga; mmoja atachukuliwa, mwingine ataachwa.
42 “Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni siku gani ataka pokuja Bwana wenu.
43 “Lakini fahamuni kwamba, kama mwenye nyumba angalifahamu ni saa ngapi za usiku ambapo mwizi atakuja, angalikaa macho asiache nyumba yake ivunjwe. 44 Kwa hiyo ninyi pia lazima muwe tayari kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja saa ambayo hamnita zamii.”
Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu
45 “Basi, ni nani mtumishi mwaminifu ambaye bwana wake amemweka awe msimamizi wa watumishi wengine nyumbani kwake, awape posho yao kwa wakati wake? 46 Heri mtumishi ambaye atakapokuja bwana wake atamkuta anafanya hivyo. 47 Nawaambieni kweli, atam fanya mtumishi huyo asimamie mali yake yote.
48 “Lakini kama mtumishi huyo ni mwovu atasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu hatarudi kwa muda mrefu,’ 49 na ataanza kuwapiga watumishi wenzake na kula na kunywa na walevi. 50 Bwana wake atakuja wakati ambapo mtumishi huyo hamtazamii na saa ambayo haijui. 51 Ndipo atamwadhibu huyo mtumishi na kumweka katika kundi la wanafiki; huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.”
Copyright © 1989 by Biblica