Old/New Testament
Ufufuo Wa Wafu
23 Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wanaoamini kwamba wafu hawafufuki, walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 24 “Mwalimu, Musa alitufundisha kwamba mtu akifariki pasipo kupata watoto, ndugu yake amwoe huyo mjane ili ampatie kaka yake watoto. 25 Hapa kwetu walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, kisha akafariki na kwa kuwa hakuwa na watoto, yule mjane alichukuliwa na ndugu yake. 26 Ikatokea hivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili hadi wote saba wakamwoa huyo mjane bila kupata watoto. 27 Baadaye, yule mjane naye akafariki. 28 Sasa tuambie, siku ile ya ufufuo, ata hesabiwa kuwa ni mke wa nani? Maana aliolewa na wote saba!”
29 Yesu akawajibu, “Mnakosea kwa sababu hamjui Maandiko wala uwezo wa Mungu. 30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa; kwa maana watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31 Na kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma Mungu alivyowaambia kwamba, 32 ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”
33 Ule umati wa watu waliposikia hayo, walishangazwa sana na mafund isho yake.
Amri Kuu Kuliko Zote
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”
37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”
Kristo Ni Mwana Na Bwana Wa Daudi
41 Mafarisayo walipokuwa pamoja Yesu aliwauliza, 42 “Mnaonaje kuhusu Kristo? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”
43 Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi anapozungumza kwa Roho anamwita Kristo ‘Bwana,’ kwa kusema, 44 ‘Bwana alimwam bia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.’ 45 Kama Daudi anamwita ‘Bwana 46 Hakuna aliyeweza kumjibu Yesu hata neno moja. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kum wuliza maswali.
Copyright © 1989 by Biblica