Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Exod for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matayo 21:1-22

Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe

21 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, aka waagiza, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu na mkiingia mtamwona punda amefungwa na mwanapunda pamoja naye. Wafungueni mniletee. Kama mtu akiwauliza lo lote, mwambieni, ‘Bwana anawa hitaji Haya yalitokea ili kutimiza utabiri wa nabii aliposema, ‘Mwambieni binti Sayuni, tazama mfalme wako anakuja kwako ni mnyenyekevu, na amepanda punda, mwanapunda, mtoto wa punda.’

Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyowaagiza. Wakamleta yule punda na mwanapunda. Wakatandika mavazi yao juu ya hao punda na Yesu akaketi juu yake. Umati mkubwa wa watu wakatandika nguo zao barabarani, wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani. Ule umati wa watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapiga kelele wakisema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi . Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Hosana juu mbin guni.”

10 Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukajawa na hekaheka, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” 11 Ule umati wa watu wakajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

Yesu Afukuza Wafanya Biashara Hekaluni

12 Yesu aliingia katika eneo la Hekalu akawafukuza wote wali okuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za watu waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13 Akawaambia, “Imeandikwa katika Maandiko, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang’anyi.”

14 Vipofu na vilema wakamwendea, naye akawaponya. 15 Lakini makuhani wakuu na walimu wa sheria waliudhika walipoona mambo ya ajabu aliyoyafanya na kuwasikia watoto wakishangilia Hekaluni wakisema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi!” Wakamwuliza Yesu, 16 “Unasikia hawa wanavyosema?” Akawajibu, “Nasikia. Kwani hamjasoma maneno haya, ‘Kutoka katika vinywa vya watoto wadogo na wale wanaonyonya umeleta sifa kamili’? ” 17 Akawaacha akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.

18 Asubuhi, Yesu alipokuwa akirudi mjini, aliona njaa. 19 Alipoona mtini kando ya bara bara aliusogelea akakuta hauna tunda lo lote ila majani tu. Akaulaani akisema, “Usizae matunda kamwe!” Wakati huo huo ule mtini ukanyauka. 20 Wanafunzi wake wakashangazwa na tukio hilo wakamwuliza, “Imekuwaje mtini huu ukanyauka ghafla?” 21 Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli, kama mna imani na msiwe na mashaka hata kidogo, mtaweza kufanya yaliy ofanyika kwa huu mtini; na hata mkiuambia mlima huu, ‘Ng’oka, nenda kajitupe baharini,’ itafanyika. 22 Na lo lote mtakaloomba katika sala, mtapewa, kama mna imani.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica